Vita ya tatu ya dunia? Baada ya mkwala wa Marekani, China yajibu mapigo

Jenerali wa ngazi za juu wa China alisema nchi yake ina haki ya kupeleka askari na silaha "katika eneo lake"

Vita ya tatu ya dunia? Baada ya mkwala wa Marekani, China yajibu mapigo

Jenerali wa ngazi za juu wa China alisema nchi yake ina haki ya kupeleka askari na silaha "katika eneo lake"

02 June 2018 Saturday 19:35
Vita ya tatu ya dunia? Baada ya mkwala wa Marekani, China yajibu mapigo

China imeyaita matamshi ya Marekani kama "yasiyo na weledi" kwamba inatisha majirani zake kwa kupelekwa majeshi yake katika Bahari ya Kusini ya China.

Jenerali wa ngazi za juu wa China alisema nchi yake ina haki ya kupeleka askari na silaha "katika eneo lake".

Waziri wa Ulinzi wa Marekani James Mattis alisema vitendo vya Beijing vinaleta maswali mengi juu ya malengo yake mapana.

Mataifa sita ya eneo hilo yana madai juu ya eneo hilo la baharini, lakini China imesisitiza madai yake kwa ujenzi wa visiwa na kufanya doria.

Jenerali Mattis alitoa maoni yake katika mkutano wa usalama nchini Singapore.

Akizungumza katika mkutano huo, Luteni Jenerali He Lei wa China alisema: "Maoni yoyote kutoka nchi nyingine hayawezi kukubalika."

Jenerali alisema kuwa kupelekwa kwa askari kulikuwa ni sera ya "ulinzi wa taifa", akiongeza: "Ina lengo la kuepuka kulivamiwa na wengine.

"Kama eneo ni lako unaweza kupeleka jeshi na silaha."

Aliongeza: "Tunaona taifa lolote ambalo linajaribu kupiga kelele juu ya hili kama linaingilia kati katika mambo yetu ya ndani."

Mattis alisema Beijing imetumia vifaa vya kijeshi, ikiwa ni pamoja na makombora ya kupambana na meli, makombora ya kutungua ndege za kivita na vifaa vya kuharibu mawasiliano ya kielekroniki katika maeneo yote ya Bahari ya Kusini ya China.

"Pamoja na madai ya China, uwekaji wa mifumo hii ya silaha unaendana moja kwa moja na matumizi ya kijeshi kwa madhumuni ya kutisha na kulazimisha wengine," alisema.

"Sera ya China katika Bahari ya Kusini ya China inatofautiana kabisa na uwazi ambao mkakati wetu unajaribu kuutangaza, inazua maswali juu ya malengo mapana ya China."

Picha za satelaiti zinaonyesha China ikipeleka wanajeshi na vifaa katika kisiwa cha Woody ambacho ni miongoni mwa visiwa vya Paracels vinavyogombaniwa.

Licha ya upinzani wake, Jenerali Mattis aliongeza kuwa Marekani "itaendelea kufuata uhusiano mzuri, unaozingatia matokeo na China" na "ushirikiano wakati wowote iwezekanavyo".

Mwezi uliopita China alisema kuwa kwa mara ya kwanza ilipeleka ndege za kijeshi kwenye kisiwa cha Woody, na kusababisha onyo kali toka kwa Marekani kuwa kitendo hicho kina lengo la kuharibu amani ya eneo hilo.

Kisiwa cha Woody, ambayo China huita Yongxing, pia kinadaiwa na Vietnam na Taiwan.

Mattis alikuwa akizungumza siku 10 kabla ya Rais Donald Trump hajakutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un huko Singapore.

Mattis alisema suala la kuondosha askari wa Marekani kutoka Korea Kusini kamwe haliwezi kufanyika na kwamba "lengo letu linabakia kuwa Korea Kaskazini kuachana kabisa na nyuklia ".

Mgogoro wa bahari ya Kusini mwa China

Utawala juu ya visiwa ambavyo kwa sehemu kubwa havijakaliwa na binadamu, vya Paracels na Spratlys, vinadaiwa na China, Vietnam, Filipino, Taiwan na Malaysia

China inadai sehemu kubwa zaidi ya eneo hilo kama lake, ikisema haki zake ni za karne nyingi nyuma - mwaka wa 1947 ilitoa ramani inayoonyesha madai yake

Eneo hilo ni njia kuu ya meli, na bahari yenye utajiri mkubwa kwa ajili ya uvuvi, na inadhaniwa kuhifadhi mafuta na gesi kwa wingi

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.