Vita ya tatu ya dunia? Serikali China yaiba siri za jeshi la Marekani

Takwimu zilizoibiwa katika tukio hilo ni pamoja na mipango ya mradi wa makombora ya kasi kuu (supersonic)

Vita ya tatu ya dunia? Serikali China yaiba siri za jeshi la Marekani

Takwimu zilizoibiwa katika tukio hilo ni pamoja na mipango ya mradi wa makombora ya kasi kuu (supersonic)

09 June 2018 Saturday 12:40
Vita ya tatu ya dunia? Serikali China yaiba siri za jeshi la Marekani

Shirika la Upelelezi la Marekani FBI linafanya uchunguzi baada ya wadukuzi wa serikali ya China kufanya udukuzi dhidi ya mkandarasi wa Jeshi la Wanamaji wa Marekani na kuiba taarifa za siri za usalama, vyombo vya habari vya Marekani vinasema.

Takwimu zilizoibiwa katika tukio hilo ni pamoja na mipango ya mradi wa makombora ya kasi kuu (supersonic), viongozi wa Marekani waliiambia Washington Post.

Shambulizi hilo, mnamo Januari na Februari mwaka huu, yalithibitishwa na CBS News.

Wadukuzi walimlenga mkandarasi anayehusishwa na shirika la Jeshi la Marekani linalohusika na utafiti na maendeleo kwa ajili ya manowari na silaha za chini ya maji.

Katika hatua nyingine, afisa wa zamani wa kijasusi wa Marekani alikutwa na hatia ya kutoa hati za siri kwa jasusi wa Kichina.

Kevin Mallory, mwenye umri wa miaka 61, alikutwa na hatia chini ya Sheria ya Upelelezi ya Marekani siku ya Ijumaa. Anatarajiwa kushtakiwa tarehe 21 Septemba na anakabiliwa na adhabu ya juu ya maisha gerezani, idara ya haki ya Marekani ilisema kupitia taarifa kwa vyombo vya habari.

Katika kesi ya mkandarasi wa Jeshi la Wanamaji wa Marekani, maafisa wa Marekani waliiambia Washington Post kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikifanya kazi katika kituo cha Naval Undersea Warfare Center, shirika la kijeshi lenye makao yake makuu huko Newport, Rhode Island nchini Marekani.

Waliongeza kuwa miongoni mwa taarifa zilizoibiwa na China ni zile zinazohusiana na mradi unaojulikana kama Sea Dragon, pamoja na taarifa zilizo ndani ya maktaba ya mpango wa kuunda manowari na vita vya kielekroniki.

Mipango ni pamoja na mfumo wa silaha za kupambana na meli ambazo zitawekwa kwenye manowari za Marekani kufikia mwaka 2020.

Ingawa taarifa zilihifadhiwa kwenye mtandao usio wa siri sana wa mkandarasi, inachukuliwa kuwa nyeti kwa sababu ya asili ya teknolojia inayoundwa na uhusiano wake na miradi ya kijeshi.

Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Marekani, Bill Speaks, alisema kuwa kuna taratibu ambazo zipo zinazozitaka kampuni kutoa taarifa serikalini wakati "tukio la shambulizi la kimyandao" limefanyika.”

"Haitokuwa sahihi kujadili kwa kina zaidi kwa wakati huu," aliongeza.

Uchunguzi unaongozwa na Jeshi kwa msaada wa FBI, maafisa walisema.

Siku ya Ijumaa, Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Jim Mattis, aliamuru mapitio katika masuala yaliyotokana na uendeshaji wa mkandarasi huyo, inaripoti CBS News, akitoa mfano wa ofisi ya mkaguzi mkuu wa Pentagon.

Habari hizi zinakuja siku kadhaa kabla ya mkutano wa kilele huko Singapore ambako Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, ambaye anaichukulia Beijing miongoni mwa washirika wake.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.