Wanawake dunia nzima sasa kuendesha magari baada ya Saudi Arabia kuondoa zuio

Saudia ni nchi pekee duniani ambako mwanamke haruhusiwi kuendesha gari

Wanawake dunia nzima sasa kuendesha magari baada ya Saudi Arabia kuondoa zuio

Saudia ni nchi pekee duniani ambako mwanamke haruhusiwi kuendesha gari

05 June 2018 Tuesday 16:09
Wanawake dunia nzima sasa kuendesha magari baada ya Saudi Arabia kuondoa zuio

Na Mwandishi Wetu

WANAWAKE wote duniani sasa kuendesha magari mara baada ya Saudi Arabia kuondoa katazo hilo na sasa imeanza kuwapatia leseni.

Taarifa zinasema kuwa Saudi Arabia ambayo lilikuwa taifa pekee lililowazuia wanawake kuendesha magari, limelainika na sasa limewaruhusu.

Tangazo hilo limekuja wiki tatu kabla ya marufuku ya wanawake kuendesha gari kuondolewa rasmi nchini humo, kufuatia uamuzi wa mwaka uliopita wa Mfalme Salman wa kuwaruhusu wanawake kuendesha gari.

Saudia ni nchi pekee duniani ambako mwanamke haruhusiwi kuendesha gari, lakini hilo linatarajiwa kubadilika ifikapo Juni 24.

Kulingana na taarifa ya Wizara ya Mawasiliano, leseni za udereva zipatazo 2,000 zitatolewa kwa wanawake wiki ijayo.

Lakini hatua hiyo nzuri imefuatiwa na kuwekwa kizuizini kwa watu 17 wiki iliyopita kwa madai ya kuhujumu usalama wa ufalme, katika kile ambacho waendesha kampeni wamesema ni ukandamizaji dhidi ya wanaharakati.

Vikundi vya kutetea haki za binadamu vimesema wafungwa ni wanaharakati wa kike wanaopigania haki ya kuendesha gari na kumaliza mfumo wa Kiislam unaomuweka mwanamke chini ya ulinzi wa mwanaume.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.