Watakiwa kuadhibiwa kwa uchochezi

Ni kwa kuchochea vita nchini Sudan Kusini

Watakiwa kuadhibiwa kwa uchochezi

Ni kwa kuchochea vita nchini Sudan Kusini

29 May 2018 Tuesday 10:22
Watakiwa kuadhibiwa kwa uchochezi

Na Mwandishi Wetu

MAAFISA sita wa Sudan Kusini huenda wakaongezwa kwenye orodha ya vikwazo vya kutosafiri kutokana na kuhusika kwao na uchochezi wa vita katika taifa hilo.

Kuongezwa kwao kunategemeana na ombi la Marekani la kulitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kufanya hivyo.

Hayo ni kwa mujibu wa rasimu ya azimio iliyoonekana na shirika la habari la Ufaransa, AFP, hapo jana.

Waziri wa ulinzi Kuol Manyang Juk yumo katika orodha hiyo kwa kukiuka makubaliano ya hivi karibuni ya kusitisha mapigano yaliyosainiwa na serkali mwaka uliopita na kwa kuongoza mashambulizi katika mji wa kaskazini mashariki wa Pagak uliotekwa na vikosi vya waasi mwaka uliopita.

Maafisa hao sita watakabiliwa na vikwazo vya kutosafiri na mali zao kuzuiwa iwapo rasimu hiyo ya azimio itaridhiwa kwenye mkutano uliopangwa kufanyika siku ya Alhamisi wiki hii.

Baraza la usalama linatarajiwa kukutana leo kujadili vikwazo vilivyopendekezwa na Marekani ambavyo vinakuja wakati serikali ya mjini Washington ikiendelea na shinikizo.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.