Waziri Mkuu aponea chupuchupu kwa kura ya kutokuwa na imani

Waziri Mkuu aponea chupuchupu kwa kura ya kutokuwa na imani

17 June 2018 Sunday 11:17
Waziri Mkuu aponea chupuchupu kwa kura ya kutokuwa na imani

Na Mwandishi Wetu

JINA la Macedonia nusura limuondoe madarakani Waziri Mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras mara baada ya upinzani kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Taarifa zinaonyesha kuwa Tsipras, amenusurika katika kura ya kutokuwa na imani dhidi yake, iliyoitishwa bungeni na upinzani kuhusu makubaliano ya kihistoria aliyofanya kumaliza mzozo wa miaka mingi na Macedonia kuhusu jina.

Wabunge 153 waliipinga kura hiyo huku 127 wakiiunga mkono. Kushindwa kwa kura hiyo kunafungua njia ya mkataba huo kusainiwa leo, hatua ambayo ni muhimu kumaliza mzozo ambao umedumu kwa miaka 27.

Mkataba huo unairuhusu nchi jirani Macedonia kuitwa Jamhuri ya Macedonia Kaskazini.

Ugiriki imekuwa katika mvutano na Macedonia tangu mwaka 1991 kuhusu jina la nchi hiyo ambayo zamani ilikuwa sehemu ya jamhuri ya Yugoslavia.

Wafuasi wa siasa za kizalendo nchini Ugiriki wanashikilia kuwa jina Macedonia ni la mkoa wa kale na wa sasa wa Ugiriki na halipaswi kutumiwa na nchi hiyo.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.