Waziri Mkuu Israel amuonya Kansela Markel kuhusu Iran

Iran ni hasimu mkubwa wa Israel katika eneo la Mashariki ya Kati

Waziri Mkuu Israel amuonya Kansela Markel kuhusu Iran

Iran ni hasimu mkubwa wa Israel katika eneo la Mashariki ya Kati

05 June 2018 Tuesday 15:33
Waziri Mkuu Israel amuonya Kansela Markel kuhusu Iran

Na Mwandishi wetu

WIMBI jipya la wakimbizi barani Ulaya linaweza kuibuka endao Iran itaendelea kuingilia kati masuala ya Masharik ya Kati, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameionya Ujerumani.

Taarifa zinasema kuwa Netanyahu ameyasema hayo wakati walipokuwa wakiujadili mustakbali wa mpango wa nyuklia na Iran.

Akianza ziara yake ya siku tatu barani Ulaya, Waziri Mkuu huyo amesema Iran imeweza kuwa na uwepo mkubwa wa kijeshi nchini Syria na Yemen kwa sababu ya kuondoshewa vikwazo ilivyokuwa imewekewa baada ya kukubali kusitisha shughuli zake za kinyuklia.

Merkel kwa upande wake ameyatetea makubaliano ya nyuklia na Iran kwa kusema kwamba shughuli za kinyuklia za nchi hiyo kwa sasa zimedhibitiwa, na kabla ya makubaliano hayo kutiwa saini Iran ilikuwa inaelekea kumiliki silaha za kinyuklia.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.