Misingi ya kujitanua katika biashara ya mtandaoni

“Biashara ya mtandaoni haihitaji uwe na mtaji mkubwa wala haihitaji kutumia nguvu nyingi, unaweza kufanya hata kwa masaa mawili ukatumia mitandao ya kijamii...

Misingi ya kujitanua katika biashara ya mtandaoni

“Biashara ya mtandaoni haihitaji uwe na mtaji mkubwa wala haihitaji kutumia nguvu nyingi, unaweza kufanya hata kwa masaa mawili ukatumia mitandao ya kijamii...

03 June 2018 Sunday 18:10
Misingi ya kujitanua katika biashara ya mtandaoni

Na Amini Nyaungo

Wakati mitandao ya kijamii na biashara ya mtandaoni ikizidi kushamiri hapa Tanzania, Juliana Raymond ameweza na amethubutu hadi kuisaidia familia yake kupitia biashara hiyo.

Juliana ameiambia Azania Post kuwa ukitaka kuanza biashara ya ‘Online’ wala usiwe na hofu unaweza ukaanza tena hata ukiwa na watu wachache ambao wataweza kukusaidia kuinuka kibiashara.

Kikubwa uwe unapatikana kikamilifu katika mitandao ya kijamii, Instagram, Twitter na Facebook. Kuhusu wanaokufuata ‘Followers’ usiwe na shaka nao kadri unavyojaribu kuweka bidhaa nzuri ndipo unapata wafuataji wengi na kuvutiwa na biashara yako.

“Biashara ya mtandaoni haihitaji uwe na mtaji mkubwa wala haihitaji kutumia nguvu nyingi, unaweza kufanya hata kwa masaa mawili ukatumia mitandao ya kijamii kuposti na kuangalia nani anahitaji,” amesema.

Kupitia kampuni yake ya Thanx Much ameweza kununua gari huku akisomesha wadogo zake wakati huo huo biashara yake imezidi kukua.

Pia anashauri usifiche sura yako wakati wa kutangaza biashara yako wala usifiche wapi unaishi kwa lengo la kuwapa Imani wateja wako.

Anapenda kuwa kama Jokate Mwegelo baada ya kuona jitihada zake za `brand` yake ya `kidoti’ na anaamini atafika.

Juliana ni miongoni mwa wasichana wachache Tanzania waliofanikiwa kuthubutu katika biashara na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Amesema kuhusu wanaume kumsumbua kupitia mitandao ya kijamii ipo na kama mwanamke lazima atongozwe ila anachokifanya kuuza bidhaa zake za Thanx Much hajiuzi yeye kama yeye. Hiyo ndiyo misingi imara kama unahitaji kuendelea katika biashara hii ya mitandaoni.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.