Umoja wa Mataifa taabani Kifedha ifikapo Agosti 2019

Umoja wa Mataifa taabani Kifedha ifikapo Agosti 2019

05 June 2019 Wednesday 18:06
Umoja wa Mataifa taabani Kifedha ifikapo Agosti 2019

Azania post / Xinhua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Jumanne iliyopita  Juni 4, 2019 ametoa wito kwa jumuia ya kimataifa kuisadia Taasisis hiyo kubwa duniani kukabiliana na uhaba wa fedha unalolikabili shirika hilo kwa sasa.

"Licha ya jitihada mbalimbali za kubana matumizi katika mwaka huu lakini bado tunakabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha itakapofika mwezi Agost 2019, hivyo tutalazimika kukopa kutoka kwenye Mfuko Mtaji wa kufanyia kazi" alisema Guterres. Alisema wakati akitoa maoni yake kwenye mkutano wa kawaida wa kamati ya Tano ya Umoja huo. Umoja wa Mataifa una raslimali nyingi kuliko matumizi yake ambazo hazitoshi kukidhi matakwa ya uendeshaji wa Umoja alisisitiza.

Kwa mujibu wa Guterres, sababu kubwa ya mdororo wa fedha kwenye Umoja huo ni kuongezeka kwa madeni yanayotokana na malimbikizo ya ada kwa nchi wanachama na madeni ya michango ya kulinda amani . Kiongozi huyo mkuu wa Umoja wa mataifa alisema malimbikizo hadi mwisho wa mwaka 2018 yalifikia dola za kimarekani milioni 529 sawa na asilimia 20 ya makadirio ya mwaka. Miezi mitano katika mwaka huu malimbikizo yamebaki dola za kimarekani milioni 492.

Updated: 05.06.2019 18:13
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.