banner58

Baiskeli yaongeza mahudhurio shule za msingi kwa asilimia 28 kusini mwa Sahara

Baiskeli yaongeza mahudhurio shule za msingi kwa asilimia 28 kusini mwa Sahara

04 June 2018 Monday 11:30
Baiskeli yaongeza mahudhurio shule za msingi kwa asilimia 28 kusini mwa Sahara

Na Mwandishi Wetu

MAHUDHURIO ya wanafunzi wengi katika nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara yameongezeka kwa asilimia 28 mara baada ya kupatiwa msaada wa usafiri wa baiskeli, imefahmika.

Kiongozi wa shirika la misaada la kimataifa, World Bicycle Relief Dave Neiswander anasema kuwa shirika lake limekuwa likiteleza mpango wa kugawa baiskeli kwa shule na watu katika nchi kadhaa.

Kutokana na mradi huo mahudhurio shuleni yameongezeka kwa asilimia 28 kwenye sehemu za mashambani katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara . Na ufanisi miongoni mwa watoto wa shule umeongezeka kwa asilimia 59.

Katika kutambua umuhimu wa chombo hicho, tayari umoja wa mataifa umetanga kila tarehe 3 Juni kuwa ni siku ya baiskeli kimataifa.

Shirika hilo la misaada ya baiskeli pia linashirikiana na wakulima wadogo wadogo na wahudumu wa afya ili kuzitatua changamoto za usafiri kwenye sehemu za mashambani. Mpaka sasa shirika hilo la misaada limeshagawa baiskeli 400,000 na pia limeshatoa mafunzo ya uhandisi wa baiskeli kwa vijana 1900 barani Afrika.

Bwana Neiswander ameongeza kusema kwamba njia rahisi ya kutumia baisikeli inaleta faida nyingi. Watoto wanawahi masomo shuleni kutokana na kutumia baiskeli na hata wakulima wanawezeshwa kuwa na njia bora ya kupeleka mazao yao kwenye masoko ili kuyauza.

Hata hivyo licha ya faida zote hizo watu mara nyingi hawaitilii maanani baiskeli kuwa kifaa cha kuleta maendeleo. Baada ya kupitisha siku ya baisikeli duniani, Umoja wa Mataifa unawataka wanachama waipe basikeli kipaumbele katika mikakati yao ya maendeleo sambamba na kuijumuisha katika maamuzi ya kisiasa na mipango ya kitaifa na kimataifa.

Mkurugenzi huyo amesema siku ya baiskeli duniani itasaidia kuhamasisha mwamko wa kutambua umuhimu wa baisikeli kijamii na kiuchumi. Ameeleza kuwa siku ya baisikeli duniani pia itachangia katika kuonyesha umuhimu wa usafiri wa baiskeli kwa kuhakikisha kwamba hakuna anaeachwa nyuma au anaeshindwa kwenda shule, hospitali au sokoni, ati kwa sababu tu sehemu hizo ziko mbali kutoka kwake

Azania Post

Updated: 04.06.2018 11:40
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.