TCU yafungua dirisha la udahili wa mosomo 2019

TCU yafungua dirisha la udahili wa mosomo 2019

16 July 2019 Tuesday 12:21
TCU yafungua dirisha la udahili  wa mosomo 2019

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
TUME ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imetangaza kufunguliwa kwa awamu ya kwanza ya  dilisha la udahili wa wanafunzi wanaotaka kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka 2019.

Vile vile TCU imetoa ruksa ya udahili kwa vyuo vilivyokuwa vimefungiwa baada ya kukidhi vigezo. Vyuo hivyo ni  Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mkuu Mihayo (AMUKTA), Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian Bagamoyo, Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji, na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (KIU).
 

Taarifa hizo zimetolewa Julai 15, 2019 na Mkurugenzi wa Uratibu na Udahili wa tume hiyo, Dk Kokuberwa Katunzi-Mollel katika Maonyesho ya TCU yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi mmoja  jijini Dar es Salaam

"Tayari  udahili kwa mwaka wa masomo 2019  umefunguliwa kwa awamu ya kwanza kuanzia  Julai 15 hadi Agosti 10, 2019 Wanafunzi wanaotaka kujiunga na elimu ya juu waanze kutuma maombi yao'' amesema na kuongeza . " Pia  baadhi ya vyuo  vilivyokuwa  vimefungiwa vimeruhusiwa kufanya udahili baada ya kukidhi vigezo vilivyotakiwa''

PICHANI; Mkurugenzi wa Uratibu na Udahili wa TCU, Dk Kokuberwa Katunzi-Mollel

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.