banner68
banner58

Wanafunzi sekondari wagoma, wataka kusaidiwa majibu ya mtihani wa taifa

Wanafunzi wakachachamaa na kuharibu mali, wakihimiza utawala wa shule kuwarudisha makwao ulipokataa kuwasaidia kuiba mitihani

Wanafunzi sekondari wagoma, wataka kusaidiwa majibu ya mtihani wa taifa

Wanafunzi wakachachamaa na kuharibu mali, wakihimiza utawala wa shule kuwarudisha makwao ulipokataa kuwasaidia kuiba mitihani

27 May 2018 Sunday 19:17
Wanafunzi sekondari wagoma, wataka kusaidiwa majibu ya mtihani wa taifa

Shule ya sekondari ya wavulana ya Ortum katika kata ya West Pokot nchini Kenya imefungwa kwa muda usiojulikana baada ya wanafunzi kugoma Jumamosi usiku, wakidai kusaidiwa katika kudanganya katika ukaguzi wa Cheti cha Elimu ya Sekondari (KCSE).

Wanafunzi wakachachamaa na kuharibu mali, wakihimiza utawala kuwapeleka nyumbani.

Mkurugenzi wa elimu ya Kaunti ya West Pokot Jared Obiero alisema alifanya mkutano na wadau wa elimu, mkuu wa shule na wanafunzi Jumamosi alasiri baada ya kupokea ripoti ya kiintalijensia kuwa wanafunzi walikuwa wamepanga mgomo wa kupinga kutopewa ushirikiano' na mkuu wao shule katika mpango wa kudanganya katika mtihani.

Kulingana na afisa huyo, wanafunzi walitaka kuwa mkuu huyo wa shule kuweka wazi msimamo wake na kuwaunga mkono kudanganya kwenye mtihani.

"Sisi tulizungumza na wanafunzi kuwaambia wanachodai hakiwezi kuvumiliwa mahali popote. Hata bado hawakuelewa. Mkuu wa shule ni mgeni na amekuwa hapa kwa wiki tatu tu. Waliendelea kumwomba kusema wazi ikiwa atawasaidia katika kudanganya kwenye mtihani," alisema.

"Mwalimu Mkuu anafundisha Fizikia kidato cha tatu. Aliwaambia kuwa anachoweza kufanya ni kuwasimamia vizuri walimu kuwafundisha na kuhakikisha wote wanahudhuria darasani," aliongeza.

Mwaka jana, matokeo ya wanafunzi 320 wa shule hiyo yalifutwa kutokana na kudanganya katika mtihani.

Mbunge wa eneo hilo Daudi David Pkosing alifungua kesi mahakamani kukataa uamuzi wa KNEC, lakini kesi hiyo ilitupiliwa mbali.

Alipotafutwa mkuu wa shule kwa ajili ya kutoa maoni yake, Bw Tiony Simon alisema haungi mkono wizi wa mtihani na aliwaeleza wanafunzi juu ya msimamo wake huo.

Alibainisha kuwa kisiasa zimechangia machafuko ya wanafunzi na kuwataka wanasiasa kuacha kujiingiza katika masuala ya shule.

"Wanasema wanataka kusaidiwa kufaulu mitihani kwa kuiba mitihani lakini niliwafukuza na kuwaambia walimu watawaandaa kwa ajili ya mitihani. Hili liliwasababisha kubadilika na wakaanza kuimba kwa sauti kwamba Tiony lazima aondoke," alisema.

Standard Media

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.