Wasio na vitambulisho vya ujasiliamali kufikishwa mahakamani

Wasio na vitambulisho vya ujasiliamali kufikishwa mahakamani

22 May 2019 Wednesday 13:49
Wasio na vitambulisho vya ujasiliamali kufikishwa mahakamani

Na Mwandishi wetu, Mbeya.
KUFUATIA kuwepo  kwa tabia ya  wajasiriamali  wadogo kukwepa kununua vitambulisho vilivyotolewa na Serikali kwa gharama ya Sh 20,000 halmashauri ya Jiji la Mbeya imetangaza kuanza msako  na kuwafikisha mahakamani watakaobainika kuendesha biashara bila ya  kitambulisho cha ujasiliamali.

Ofisa habari Jiji la Mbeya John Kaluwa amesema ofisini  kwake  leo Mei 22, 2019  kuwa wameamua kufanya msako huo baada ya kubaini kuwepo kwa baadhi ya wafanyabishara kuwa na mchezo mchafu wa kutumia kitambulisho kimoja kwa watu zaidi ya watatu jambo lililokwamisha kutofikia malengo waliyokusudia.

"Tumebaini kuwa  Jiji lina wafanyabishara wengi lakini idadi walionunua vitambulisho ni wachache na hivyo tumeona sasa ni vyema kufanya msako wa kuhakikisha tunawabaini, hususan kwa wale ambao hawana vitambulisho," alisema.

Amesema lengo la Serikali kuwataka kila mfanyabishara kununua kitambulisho kwa bei ya Sh 20,000 ni kuondoa ushuru wa kila siku na hivyo sasa ni vyema wakatii sheria bila shuruti kabla ya mkono wa sheria kuchukua mkondo wake.

Mfanyabishara wa Matunda  Jijini hapa Anna Sanga , ameomba  uongozi wa jiji kuona namna  ya kuwasaidia kutokana na kuwepo na mitaji midogo ambayo hailingani na gharama za malipo ya vitambulisho vya wajasiriamali.

Amesema  mtaji wake ni  Sh 5,000 na kwamba kitendo cha kulipia kitambulisho kwa gharama ya sh,20,000 kitamlazimu kuingia katika madeni ambayo baadaye yatamgharimu kurejesha.

Mfanyabishara wa Viatu vya Mitumba, Joseph Athony  amesema kuwa  mfumo huo umekuja haraka sana na kwamba serikali ilipaswa kutoa elimu ya umuhimu wa kuwa na vitambulisho vya ujasirimali ili kuwawezesha kujiandaa na kulimbikiza fedha ili wasiweze kukinzana na maagizo ya Serikali.
Updated: 22.05.2019 14:00
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.