banner68
banner58

Diamond, Nandy  wakamatwa  na kuhojiwa  polisi kwa kupost picha zisizo na maadili

Diamond, Nandy  wakamatwa  na kuhojiwa  polisi kwa kupost picha zisizo na maadili

17 April 2018 Tuesday 11:07
Diamond, Nandy  wakamatwa  na kuhojiwa  polisi kwa kupost picha zisizo na maadili

Na Mwandishi Wetu

MWANAMUZIKI maarufu nchini Tanzania  Diamond Platnumz na mwimbaji nyota  Faustina Charles maarufu kama Nandy wamekatwa na kuhojiwa na polisi mara baada ya kupost kwenye mitandao picha zinazokiuka maadili, Bunge limeelezwa mjini Dodoma leo.

Hayo yamesemwa na Waziri  wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ulanga Goodluck Mlinga (CCM) aliyetaka kujua hatua ambazo serikali imechukua kutokana na watu wanaopost picha zisizo na maadili kwenye mitandao.

“Mheshimiwa spika naomba kujua kuhusu ushoga na usagaji katika mitandao ya kijamii kuna mashoga wanajitangaza kabisa mara kuna team Wema Zari na team Shilole wote wanatukana matusi kupitia mitandao. Je nini kauli ya serikali?” alihoji Mbunge huyo.

Akijibu, Waziri Mwakyembe alisema kuwa kufanya hivyo ni kinyume na maadili na tayari serikali imewachukulia hatua baadhi ya wasanii watu waliojihusisha na vitendo hivyo.

“Napenda kulitaarifu Bunge hili kuwa jana tumemkata Diamond anahojiwa na polisi kutokana na picha zake alizotuma mtandaoni, pia mwanamuziki Nandi naye anahojiwa kwa suala hilo hilo, alisema.

Waziri huyo alisema serikali haitosita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayeendelea kufanya vitendo vya kukiuka maadili kwenye mitandao na sehemu nyingine.

Azania Post

Updated: 17.04.2018 12:37
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.