R kelly aswekwa lupango ya peke yake

R kelly aswekwa lupango ya peke yake

20 July 2019 Saturday 08:24
R kelly aswekwa lupango ya peke yake

Washington, Marekani
MAHAKAMA moja nchini Marekani imempeleka lupango msanii nguli wa miondoka ya RnB, R Kelly.

Msanii huyo amefungwa jela ya peke yake bila kuchanganywa na wafungwa wengine uamuzi ambao umemfurahisha R Kelly 

Pia hata mwanasheria anayesimamia kesi inayomkabili R Kelly ya uzalilishaji kingono, Nicole Blank Becker amesema ni maamuzi mazuri na kwamba yanaepusha jambo lolote ambalo lingeweza kumtokea kama angechanganywa na wafungwa wengine.

Jumanne Julai 16,2019  R Kelly alinyimwa dhamana baada ya kukana mashtaka yote yanayomuandama ya kuwanyanyasa kingono mabinti wadogo.

Mwezi Mei, 2019 R Kelly alikamatwa  na kushtakiwa kwa tuhuma za kuhusika na makosa 11 ya unyanyasaji wa kingono ambapo kati ya makosa hayo yalikuwemo yanayohusisha kifungo cha hadi miaka 30 jela.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.