Wajapan 'wamvuruga' Kim Kardashian West

Wajapan 'wamvuruga' Kim Kardashian West

02 July 2019 Tuesday 08:45
Wajapan 'wamvuruga' Kim Kardashian West

MWANAMITINDO  Kim Kardashian West anajipanga kubadilisha jina la nguo zake za ndani kufuatia shutuma kali za kudumisha mila.

Raia wa Japani wanaotumia mitandao ya kijamii walishutumu vikali jina la kibiashara la nguo hizo, Kimono.

Kimono ni jina la vazi la taifa na kitamaduni nchini Japani.
Awali Bi Kardashian, alijitetea na kusema hatobadili jina hilo, akisema halikuwa lengo lake kukashifu vazi au utamaduni wa jamii fulani.

Lakini leo Jumanne Julai 2, 2019, amesema kuwa atatangaza jina lengine la nguo hizo hivi karibuni.

Nyota huyo wa Televisheni, mwanamitindo na mbunifu wa mavazi ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa: "Kila siku nasikiliza watu, najifunza na kukua… Nilipotangaza jina la nguo zangu, nilifanya hivyo nikiwa na nia njema moyoni."  Ameongeza: "Baada ya kufikiria kwa kina, nitazizindua kwa jina jipya tena."

Kimono, ambalo ni vazi refu kama gauni linalofungwa na mshipi, limekuwa vazi rasmi la taifa la Japani toka Karne ya 16, na linaendelea kuwa vazi rasmi la taifa hilo.

Yuka Ohishi, mwanamke raia wa Japani wiki iliyopita aliiambia BBC kuwa: "Tunavaa kimono kusherehekea afya, kukua kwa watoto, pamvu, mahafali, ndoa na misiba. Ni vazi la sherehe toka jadi na jadi.

"Hizo nguo zake za ndani hazifanani kabisa na kimono - amechagua jina hilo kwasababu ndani yake kuna Kim - hakuheshimu kabisa vazi hilo lina maana gani kwenye utamaduni wetu."
 

Updated: 02.07.2019 08:56
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.