Awashtaki majirani kwa kuchoma nyama

Awashtaki majirani kwa kuchoma nyama

03 September 2019 Tuesday 14:47
Awashtaki majirani kwa kuchoma nyama

MWANAMKE mmoja nchini Australia amejaribu kuwazuia majirani zake kuchoma nyama kwa kuwashtaki mahakamani.

Cilla Carden kutoka jiji la Perth, Magharibi mwa Australia amedai kuwa shughuli zao za uchomaji nyama, uvutaji wa sigara na kelele za watoto unavunja sheria za makazi ya watu.

Amefuata njia hiyo ya kisheria ili shughuli hizo ziache kufanywa na majirani.

Mahakama ya jimbo imetupilia mbali madai yake kwa kusema kuwa hayana maana na ushahidi wa kutosha.

Madai yalihusisha pia familia zinazoishi jirani yake kupunguza mwanga wa taa zao, kuwanyamazisha wanyama wanofuga pamoja na kuweka miti kwenye bustani zao za kupumzika.

Amesema kuwa harufu ya moshi wa sigara na nyama choma zimemsababishia ashindwe kuishi vizuri.

''Siwezi kufurahia sehemu yangu ya kupumzika. Wameweka jiko la nyama choma ili nifikiwe na harufu ya samaki - harufu pekee ninayoipata ni ya samaki tu,'' Cilla Carden ambaye hali nyama aliiambia runinga ya Nine news siku ya Jumatatu.

Uongozi wa jimbo hilo ulimjibu kuwa familia hizo zinajaribu kuishi kama familia. Hata hivyo familia waliokua wakilalamikiwa wamehamisha jiko lao la kuchomea nyama kama sehemu ya kumsaidia mlalamikaji.

Mahakama iliongeza pia familia hiyo, wamekua hawawashi taa usiku na kuwazuia watoto kucheza kutokana na hofu walioipata kwa kushtakiwa.

Bi Carden alikata rufaa ya uamuzi huo katika mahakama kuu ya Australia Magharibi, alikabidhi kurasa zaidi ya 400 zenye malalamiko ya kukata rufaa mwezi Machi.

Mwanasheria mkuu wa Mahakama hiyo alisema kuwa kurasa zilikabidhiwa kwa mahakama zinashangaza.

"Hawaruhusu watoto wao kutoka nje usiku. Hawajawasha taa kwa siku kadhaa wakiogopa hatua atakazozichua mlalamikaji na jirani yao. Hili halikubaliki," amesema Mwanasheria.

Mwezi Julai mahakama iliamua dhidi ya mlalamikaji wakisema malamishi yake yamekuwa mzigo mzito kwa majirani.

Bi Carden amesema kuwa atachukua hatua zaidi katika mahakama nyingine.

BBC

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.