Darubini kudhibiti joto la anga yazinduliwa

Darubini kudhibiti joto la anga yazinduliwa

14 July 2019 Sunday 08:32
Darubini kudhibiti joto la anga yazinduliwa

MOJAya safari muhimu zaidi za kisayansi nchini Urusi kuwahi kushuhudiwa katika baada ya utawala wa utawala wa Kisovieti imezinduliwa kutoka eneo la Baikonur.

Spektr-RG telescope chenye darubini ya anga za mbali -ni uvumbuzi uliokamilika kwa ushirikiano na Ujerumani ambayo inatarajia kupima nishati ya joto kote angani na kutoa taarifa.

Watafiti wanasema taarifa hii itasaidia kupata muundo wa dunia kwa upana zaidi. Matumaini ni kwamba Spektr-RG kitaweza kutoa mtizamo mpya juu ya upana wa anga.

Kinatarajiwa pia kutambua idadi ya mpya ya vyanzo vya nishati , kama vile mashimo makubwa meusi yaliyopo katikati mwa nyota nyingi.

Wakati gesi inapoanguka katika mashimo hayo , huwa na joto kali na kumeguka na kugeuka kuwa joto kali. Mionzi yake hatimae husababisha hali mbaya ya joto kwa dunia.

Darubini ya Spektr-RG inatarajiwa kugundua labda mashimo milioni tatu makubwa sana meusi angani wakati wa itakapokuwa angani hadi mwisho wa maisha yake.

Darubini hiyo inazunguka juu ya uzio (orbit) uliopo kwenye roketi ya Proton ambayo iliondoka Baikonur Cosmodrome eneo la Kazakhstan saa sita na dakika 31 kwa saa za Kazakhstan.

Itachukua hata hivyo wiki nyingi kabla ya darubini hiyo kuanza kazi yake.

Chombo hicho cha anga za mbali kitatakiwa kusafiri katika eneo linalochunguzwa zaidi yapata kilomita milioni 1.5 kutoka duniani linalofahamika kama -Lagrange Point 2.

Ni hapa ambapo chombo cha Spektr-RG kinaweza kupata mazingira thabiti bila kuwa nakivuli na kuyumbishwa na joto ambalo vinginevyo lingekipata kama kingekuwa karibu na sayari yetu dunia.

Spektr-RG kimetengenezwa kwa muundo wa darubini mbili kwa pamoja.

Chumba kinachochukua nafasi kubwa katika chombo hiki cha darubini ya anga za mbali, ukipenda spacebus au chassis, ni mfumo uliotengenezwa Ujerumani wa eRosita na karibu yake umefungwa na kifaa cha kisayansi kilichotengenezwa na Urusi kinachofahamika kama ART-XC.

Vifaa vyote hutumia kundi la muduli za kioo kudhibiti nguvu za mwangaza kwenye kamera za ung'amuzi.

eRosita na ART-XC zitachukua ramani ya miale kadri inavyosambaa angani katika ukubwa wa nguvu za kati ya 0.2 hadi 30 katika kipimo cha nguvu za kasi ya nishati ya anga- kiloelectron volts (keV).

Katika kipindi cha miezi sita, watatakiwa kuwa waChombo cha anga cha China huenda kikadondoka ''karibuni'' mekamlishia uchunguzi wa anga yote, ambao utarudiwa tena na tena kupata usahihi wa taarifa.

Wanasayansi wanatarajia taarifa/data zitafichuliwa. Vipimo vitakapokamilika, uchunguzi unaweza kuendela kwa kuchukua nakili za picha ya anga.

Lengo kuu la chombo cha Spektr-RG litakuwa ni kuchunguza sehemu za anga zinazotambuka kama ''kitu cheusi'' au "nishati nyeusi".

Sehemu hii ya anga inachukua hadi 96% ya shemu ya uwiano wa dunia/ni. Ufahamu wa Spektr-RG utatokana na picha ya ramani ya mgawanyo wa joto kali la inayochoma linalotolewa angani.

BBC

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.