Kuku (Jongoo) ashtakiwa, afikishwa mahakamani

Kuku (Jongoo) ashtakiwa, afikishwa mahakamani

05 July 2019 Friday 09:05
Kuku (Jongoo) ashtakiwa, afikishwa mahakamani

Paris, Ufaransa
JONGOO aliyepewa jina la Maurice amefikishwa mahakamani nchini Ufaransa akidaiwa kuwa amekuwa kero kwa majirani kwa kuwika kila alfajiri.

Analaumiwa kwa kusababisha kalele na familia moja katika kisiwa cha Oléron huko Ufaransa.

Mmiliki wake, Corinne Fesseau, anasema jogoo Maurice anafanya kile majogoo wote wanafanya 'kuwikaa'.

Waliomshtaki Maurice na Maurice mwenyewe hawakufika mbele ya mahakama ya mji wa magharibi wa Rochefort siku ya jana Alhamisi Jukai 4, 2019 kesi ilipoanza kusikilizwa.

Lakini jogoo huyo ambaye amekuwa maarufu kutokana na kesi inayomkabili, amepata uungwaji mkono kutoka kwa wafugaji kuku wengine ambao walikusanyika nje ya mahakama.

Walalamikaji, Jean-Louis Biron na Joëlle Andrieux, walijenga nyumba yao mapumziko katika kijiji cha Saint-Pierre-d'Oléron karibu miaka 15 iliyopita, lakini baadae wakaigeuza kuwa nyumba ya kuishi walipostaafu.

Sababu moja iliyowafanya kuchagua sehemu hiyo ni utulivu wake lakini tatizo ni kuwa jogoo Maurice, amekuwa kero kwao kwani amekuwa akiwapigia kelele kila alfajiri anapowika.

Wanasema tatizo hilo lilianza tangu mwaka 2017 jirani yao alipomnunua.

Walipowasilisha malamiko yao kwa Bi Fesseau, ambaye ameishi Oléron kwa miaka 35, mabishano makali yalizuka mpaka mzozo kati yao ukagonga vichwa vya habari ulipofikishwa mahakamani.

Bi Fesseau, na majirani zake wengine, walisema hakuna mjadala kuhusu swala hilo - kwa sababu ufugaji wa kuku ni sehemu ya maisha ya vijijini na kwamba hawaelewi kwa nini walalamishi wanaomba jogoo huyo azuiliwe kuwika.

Utatuzi wa mzozo huo unasubilia uamuzi wa  mahakama ambayo inatarajia kutoa hukumu ya kesi hiyo  mwezi Septemba, 2019

PICHANI, Corinne Fesseau akiwa na jogoo wake, Maurice

BBC

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.