Magari yanayotumia mafuta ya dizeli kuondolewa Ufaransa 

Magari yanayotumia mafuta ya dizeli kuondolewa Ufaransa 

03 July 2019 Wednesday 14:09
Magari yanayotumia mafuta ya dizeli kuondolewa Ufaransa 

Paris, Ufaransa
NCHI ya Ufaransa inatarajia kuyaondoa katika matumizi  magari yote yanayotumia mafuta ya dizeli nchini humo.

Hatua hiyo ni mpango mkakati wa kutunza mazingira na  kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa  yanayotokea nchini humo na Duniani kwa ujumla

Kufuatia uamuzi huo takribani magari milioni 2.76 kati ya milioni nane yaliyosajiliwa nchini humo kuanzia Januari 1997 hadi Disemba 31, 2000 hayatoruhusiwa kuendeshwa tena

Wenye magari watakaovunja sheria watatozwa faini ya euro 68 sawa na dola za kimarekani 77 huku wenye mabasi na malori watalipishwa faini ya euro 135. 

Waangalizi wa uchafuzi wa mazingira katika jiji la Paris wametaja kuwa magari yamechangia  kwa kiasi  uchafuzi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi kuanzia mwaka 2018 

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.