Merkel aitolea uvivu Italia kuhusu deni inalodaiwa

Merkel aitolea uvivu Italia kuhusu deni inalodaiwa

03 June 2018 Sunday 14:59
Merkel aitolea uvivu Italia kuhusu deni inalodaiwa

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Italia chini ya Waziri Mkuu mpya Giuseppe Conte haina jinsi kwani italazimika tu kulipa madeni yake inayodaiwa na Jumuiya ya Ulaya.

Imeripotiwa kuwa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amempongeza waziri mkuu huyo mpya. Hata hivyo ameonekana kupuuza wito ya Italia kutaka Umoja wa Ulaya kuisamehe madeni yake yanayokadiriwa kufikia euro bilioni 250

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alifanya mazungumzo na waziri mkuu mpya wa Italia Giuseppe Conte jana Jumamosi na kumkaribisha mjini Berlin kwa mazungumzo zaidi kuhusu mustakabali wa uhusiano wa nchi zao.

Kwenye tarifa, ofisi ya kansela imesema Merkel alimpongeza Conte kwa kuwa waziri mkuu. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Merkel na Conte walizungumza kwa njia ya simu, walitilia msisitizo umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa pande zote mbili.

Conte ambaye ni profesa wa shera asiyejulikana sana, amekuwa kimya tangu alipoapishwa Ijumaa. Lakini alitangaza kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa, kando na Merkel pia alizungumza na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron siku ya Jumamosi.

Amesema atakutana na viongozi hao wiki ijayo katika mkutano wa kilele wa G7 utakaofanyika Canada, ambapo pia atazungumzia masilahi ya raia wa Italia.

Bibi Merkel amesalia miongoni mwa sauti za chini kuhusu serikali mpya ya mseto nchini Italia yenye vyama viwili visivyopendelea Umoja wa Ulaya, vuguvugu la Nyota-5 na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia League.

Vyama hivyo vilifanya kampeni ambazo zilijawa ukosoaji mkubwa kwa Umoja wa Ulaya na kanda ya yuro. Kinachosubiriwa ni kuona jinsi ambavyo vyama hivi ambavyo sasa viko madarakani vitaendeleza vita vyao Brussels na Frankfurt.

Utulivu wa bibi Merkel haujaakisiwa kwingineko ndani ya Ujerumani. Katika toleo la hivi karibuni la jarida la Der Spiegel lililochapishwa Ijumaa, kwenye ukurasa wake wa mbele, jarida hilo lilikuwa na mchoro wa umma uliojaa spaghetti huku imefungiwa kamba ya kujitia kitanzi. Kichwa cha jarida kiliandikwa "Italia yajiangamiza yenyewe- na inavuta Umoja wa Ulaya pia.

Punde baada ya kuzungumza na Conte, ripoti ziliibuka kuwa Merkel anaonekana kuondoa uwezekano wowote wa Umoja wa Ulaya kuiondolea Italia madeni.

Merkel amesema ushirikiano wa Umoja wa Ulaya haupaswi kuugeuza umoja huo kuwa wa kugawana madeni bali unapaswa kusaidia wanachama ili wajisaidie wenyewe.

Azania Post

Updated: 03.06.2018 15:30
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.