Merkel atoa kali mpya ya mwaka kuhusu G7

Ameliambia bunge la Ujerumani kuwa maamuzi ya Trump kujiondoa katika mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris na wa nykulia wa Iran na kutangaza ushuru...

Merkel atoa kali mpya ya mwaka kuhusu G7

Ameliambia bunge la Ujerumani kuwa maamuzi ya Trump kujiondoa katika mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris na wa nykulia wa Iran na kutangaza ushuru...

07 June 2018 Thursday 09:43
Merkel atoa kali mpya ya mwaka kuhusu G7

Na Mwandishi Wetu

KANSELA wa Ujerumani, Angela Merkel ametoa kali ya mwaka baada ya kusema mkutano wa kilele wa nchi saba zenye nguvu duniani G 7 wiki ijayo kuwa ni “mazungumzo yenye utata”.

Kauli hiyo ameitoa ikizingatiwa tofauti zilizopo za Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu biashara, mabadiliko ya tabianchi na usalama.

Akizungumza siku mbili kabla ya mkutano huo wa Canada wa kundi la mataifa makubwa yaliyostawi kiviwanda, Merkel pia amesema viongozi hao huenda wasikubaliane kuhusu taarifa ya mwisho ya pamoja.

Ameliambia bunge la Ujerumani kuwa maamuzi ya Trump kujiondoa katika mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris na wa nykulia wa Iran na kutangaza ushuru mkubwa kwa bidhaa za chuma cha pua na bati yanaonyesha kuwa kuna tatizo kubwa katika makubaliano baina ya nchi na ndio maana kutakuwa na majadiliano yenye utata.

Merkel ameapa kuingia katika mazungumzo hayo kwa nia njema lakini akasisitiza kuwa taarifa ya mwisho kutoka kwa mwenyeji Canada, badala ya tamko la pamoja la washiriki, huenda ikawa njia pekee ya uaminifu zaidi.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.