Rais wa zamani wa Ufaransa afariki dunia

Rais wa zamani wa Ufaransa afariki dunia

26 September 2019 Thursday 14:09
Rais wa zamani wa Ufaransa afariki dunia

RAIS wa zamani wa Ufaransa, Jacques Chirac amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 86.

Chirac ambaye miaka ya baadae ilikabiliwa na kashfa za ufisadi alifariki mapema leo asubuhi Septemba 26, 2019 akiwa na familia yake , mwanawe wa kambo aliambia chombo cha habari cha AFP.

Chirac alihudumu miaka miwili kama rais wa Ufaransa na kuliongoza taifa lake kuingia katika sarafu moja ya Ulaya.

Bunge la Ufaransa limempatia heshima ya dakika moja kwa kunyamaza.

Rais wa tume ya Ulaya na waziri mkuu wa zamani wa Luxembourg Jean-Claude Juncker amesema kwamba amesikitishwa na habari hiyo.

Ulaya haikupoteza tu kiongozi muhimu ,bali idara ya urais itamkosa rafiki mkubwa, msemaji wa Juncker alinukuliwa akisema.

Mabadiliko makubwa ya kisiasa yaliofanywa na Chirac ilikuwa kupunguza muhula wa rais kutoka miaka saba hadi mitano.

Mwaka 2003 aliisaidia Marekani kuivamia kijeshi Iraq .Alihudumu kama kiongozi wa taifa kutoka 1995 hadi 2007 huku afya yake ikidorora tangu wakati huo.

Updated: 26.09.2019 14:13
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.