Waziri: Matusi yanaboresha afya 

Waziri: Matusi yanaboresha afya 

06 July 2019 Saturday 07:38
Waziri: Matusi yanaboresha afya 

Ukraine
PENGINE sote tumewahi kutukana katika maisha yetu. Ima ni kutokana na hasira au kwa sababau yoyote ile nyingine, lakini ni sehemu nzito ya lugha inayotumika na watu katika makabila tofauti.

Nchini Ukraine, kaimu waziri wa afya, Dk  Ulana Suprun amesema matusi ni mazuri kwa afya  kutokana na kwamba mtu anapotusi, inaashiria uhusiano mzito ulioimarika na ni 'mawasiliano mazuri ya kihisia' baina ya watu.

Suprun alikuwa anazungumzia sheria iliyopendekezwa ya kusitisha lugha chafu katika vyombo vya habari.

Sheria hiyo inaeleza kwamba watu wanaotukana hewani na katika hotuba kwa umma, watatozwa faini ya hadi dola  za kimarekani 49.

Lakini mtazamoa wa Dk Suprun ni kwamba kutukana au matusi ni muhimu katika hali mbaya akisema "katika visa kadhaa matusi humaanisha watu wana ukaribu na kwamba kuna mawasiliano mazuri ya kihisia kati yao".

Ameongeza kwamba ni muhimu watu kushirikiana kuondosha hamaki badala ya matusi. Licha ya sheria hiyo kulengwa kwa viongozi wa umma na sio raia wa kawaida, wengi wamefanya mzaha katika mitandao ya kijamii kuhusu namna ambavyo maisha yao yatabadilika kutokana na hilo.

Wengine wamewaza iwapo kutaidhinishwa sehemu maalum ambapo watakuwa wanaruhusiwa kutusi.

Huenda "vyumba vya kutusi " vikaidhinishwa, anapendekeza kuwepo sehemu maalum katika migahawa kwa wavutaji sigara, na wasiovuta na kadhalika kwa wanaotusi.

Sheria ya 'kuthibiti matusi' kwa sasa inajadiliwa na kamati ya bunge.

PICHANI; Kaimu waziri wa afya nchiniUkraine, Ulana Supru

BBC

Updated: 06.07.2019 07:53
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.