9 wakamatwa wakiandamana jijini Dar es Salaam

9 wakamatwa wakiandamana jijini Dar es Salaam

26 April 2018 Thursday 17:11
9 wakamatwa wakiandamana jijini Dar es Salaam

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kukamatwa kwa watu 9 waliokuwa wakiandamana eneo la Samora Avenue, Posta.

Watu hao wamekamatwa baada ya Jeshi la Polisi kuonya kuwa litawachukulia hatua kali wale wote watakaokaidi agizo la kutoandamana.

Watu hao walikuwa wakiandamana kufuatia maandamano yaliyohamasishwa kupitia mitandao ya kijamii yeye lengo la kupinga baadhi ya mambo yanayofanywa na serikali.

Mbali na watu hao, baadhi ya maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam leo yamekuwa na watu wachache sana tofauti na siku nyingine za mapumziko, ambapo watu wengi wamekuwa na hofu ya kutoka, kutokana na tetesi za kuwapo kwa maandamano.

Dar24

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.