Afisa TRA apandishwa kortini

Afisa TRA apandishwa kortini

09 September 2019 Monday 14:30
Afisa TRA apandishwa kortini

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Afisa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Peter Mwangamilo kwa kushawishi rushwa ya Sh 500,000.

Wakili wa Takukuru, Veronica Chimwanda Leo Septemba 9, amedai mbele ya Hakimu Mfawidhi, Martha Mpaze kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Septemba 3,2019.

Chimwanda amedai siku hiyo ya tukio mshtakiwa huyo alimshawishi Leonard Ruvumwa kutoa kiasi hicho cha Fedha ili kuweza kurahisisha zoezi la uhakiki kwa kampuni ya kutoa na kupokea mizigo ya Maltlines International Tanzania.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa alikana na upande wa mashtaka alidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Hata hivyo Hakimu Mpaze akitoa masharti ya dhamana alimtaka mshtakiwa huyo kuwa na mdhamini mmoja ambaye anaaminika ambaye atasaini bondi ya milioni moja.

Hata hivyo mshtakiwa huyo alifanikiwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana na kuachiwa huru.

Hakimu Mjaya aliiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 30, mwaka huu kwa ajili ya kuitaja kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.