Afisa usalama, mwenzake wafikishwa kortini

Afisa usalama, mwenzake wafikishwa kortini

02 October 2019 Wednesday 15:31
Afisa usalama, mwenzake wafikishwa kortini

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

AFISA Usalama mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, George Mwamgabe (44) na Dereva Abraham Msimu (54) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa mawili ikiwemo kusafarisha dawa za kulevya aina ya Bangi gramu 125.

Leo Oktoba 2, 2019 washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na Wakili wa Serikali, Adolf Lema mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mbando.

Katika shtaka la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Bangi zenye uzito wa gramu 125, wanadaiwa kutenda kosa hilo Agosti 25, 2018 katika eneo la Posta, Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Kosa lingine ni kusafirisa dawa za kulevya aina Heroine Hydrochloride zenye uzito wa gramu 1.55 na kuwa walilitenda kosa hilo Agosti 25, 2018 katika jijini Dar es Salaam.

Washtakiwa wamekana makosa hayo na upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Washtakiwa hao wameomba wapatiwe dhamana ambapo wamepewa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya milioni tano kila mmoja na mmoja wa wadhamini atoke Ofisi ya Umma.

Hata hivyo wameshindwa kutimiza masharti hayo, wamerudishwa rumande na kesi imeahirishwa hadi Oktoba 16, 2019.

Updated: 02.10.2019 15:39
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.