Afumaniwa, auawa

Afumaniwa, auawa

25 June 2019 Tuesday 12:13
Afumaniwa, auawa


Na mwandishi wetu, Shinyanga
MWANAUME, Shija Mahohiga(45) ameuawa baada ya kufumaniwa na mke wa mtu, Maria Kija akiwa ndani ya nyumba.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Richard Ubwao amesema tukio hilo limetokea Juni 21, 2019 katika kitongoji cha Mwasele B mji mdogo wa Mhunze wilayani Kishapu.

Amesema katika purukushani Maria alijeruhiwa na amelazwa katika hospitali ya Jakaya wilayani Kishapu.

Kamanda Ubwao amesema jeshi linamshikilia mume wa Maria ambaye ni mtuhumiwa wa mauaji hayo na mkazi wa mji huo  na kwamba atafikishwa mahakamani.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.