Afya ya Maria Nyerere yaimarika

Afya ya Maria Nyerere yaimarika

08 June 2019 Saturday 17:46
Afya ya Maria Nyerere yaimarika

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

HALI ya afya ya mke wa zamani wa rais wa Tanzania, Maria Nyerere imezidi kuimarika.

Hatua hiyo inafuatia Juni 6, 2019 kurejeshwa kwa ndege maalumu kutoka nchini Uganda alikokuwa katika ibada ya sherehe  za siku ya mashahidi  na afya yake kuzorota.

Leo Juni 8,2019 Mke wa rais Magufulu, Janeth Magufuli amemtembelea katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam  kumjulia hali na kwamba afya yake inaimarika tofauti na alivyorejea nchini.

Rais wa Uganda ,Yoweri Museveni  ndiye aliyetoa ndege rasmi ya kumrejesha nyumbani Maria Nyerere ambaye kila mwaka hudhuru nchini Uganda kwa ajili ya ibada hiyo inayofanyika Namugongo

Rais Museveni ariripotiwa kutohudhuria sherehe za siku ya mashahidi wa Uganda katika eneo la Namugongo kwa ajili ya kumtembelea Mama Maria mjini Kampala katika  moja ya hospitali mjini humo.

Updated: 09.06.2019 14:20
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.