Ajali ya moto Morogoro wengine saba wafariki dunia

Ajali ya moto Morogoro wengine saba wafariki dunia

15 August 2019 Thursday 10:54
Ajali ya moto Morogoro wengine saba wafariki dunia

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

AJALI ya mlipuko wa lori la mafuta mjini Morogoro inaendelea kugharimu maisha ya watu na hivi sasa waliofariki kutokana na mkasa huo wa Agosti 10, 2019 imefikia 89.

Idadi hiyo imeongezeka baada ya majeruhi saba kati ya wale 32 waliokuwa wamelazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) kuaga dunia.

Awali idadi ya majeruhi 46 walisafirishwa kutoka Morogoro mpaka Muhimbili kwa matibabu ya kibobezi na sasa wamebaki 25.

Mpaka kufikia jana mchana Agosti 14, 2019, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa Muhimbili, Amini Algaesha idadi ya majeruhi waliokuwa wamebakia hospitalini hapo ni 32, kati yao 17 waliku kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na sasa wamebaki 16 wakiwa ICU

Wengi wa majeruhi waliokimbizwa Muhimbili walikuwa wameunguzwa na moto kwa asilimia 80 na kuendelea.

Agosti 10, 2019 watu 62 walithibitishwa kufariki siku ya mkasa na zaidi ya 70 kujeruhiwa, na toka hapo idadi ya vifo imekuwa ikiongezeka taratibu.

Mkasa huo ulitokea majira ya saa mbili asubuhi ya Jumamosi baada ya lori lililobeba shehena ya petroli kuanguka katika mji wa Morogoro, na watu kuanza kuchota mafuta yaliyomwagika kisha mlipuko mkubwa kutokea.

Updated: 15.08.2019 12:37
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.