Alichokisema msemaji mkuu wa serikali hiki hapa

Alichokisema msemaji mkuu wa serikali hiki hapa

03 October 2019 Thursday 16:36
Alichokisema msemaji mkuu wa serikali hiki hapa

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MSEMAJI Mkuu wa serikali na kurugenzi mkuu wa Idara Habari Maelezo, Dk Hassan Abass leo Oktoba 3, 2019 jijini Dar es Salaam amezungumza mambo mbalimbali yanayohusu nchi

Haya ndiyo yaliyoajiri katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 3, 2019:

# Kwa niaba ya Serikali tunawashukuru Watanzania wote kwa kuendelea kuenzi amani lakini pia kulipa kodi na juzi tu tumesikia TRA wametangaza tumepata TZS Trilioni 1.7 kwa mwezi ambayo imevunja rekodi tangu uhuru.

# Ripoti ya Septemba 6, 2019 ya Benki ya Dunia, imeeleza kuwa Tanzania imeongoza kwa kupunguza umaskini miongoni mwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

# Awali Julai, 2019 ripoti nyingine ya WB “Human Capital; The Real Wealth of Nations” imeonesha umaskini nchini umepungua kutoka 34.4% hadi 26.8%.

# Mwezi huu pia mchango wa Tanzania katika Jumuiya ya Kimataifa na mataifa mengine umeendelea kutambulika baada ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Salim Ahmed Salim, kuwa Mwafrika wa Kwanza kupewa Tuzo ya Urafiki ya China (Friendship Award).

# Kazi kubwa imefanyika ambapo zaidi ya miradi 289 na vituo zaidi ya 89,780 vimekamilika ambapo Serikali imetumia zaidi ya TZS Bilioni 336.15.

# Kazi kubwa inaendelea kutekelezwa ambapo miradi mbalimbali vijijini ikiwemo kukamilisha vituo 44,590 vya maji.

# Hadi Septemba mwaka huu zaidi ya miradi mikubwa 17 ya maji imekamilika ambapo zimetumika zaidi ya TZS Bilioni 823.61. Wakati miradi mingine mikubwa zaidi ya 35 ya maji ikiendelea kukamilishwa nchini.

# Wastani wa upatikanaji wa maji safi mijini umefikia asilimia 80.

# Serikali iliamua kutumia zaidi ya TZS BILIONI 720 kununua korosho yote takribani tani 225,105 (ikijumuisha tani 2,139 zilizoingia kwenye maghala awali) kwa kutoa bei nzuri ya mpaka TZS 3,300 kuliko TZS 1,500 kwa kilo waliyokuwa walaliwe wakulima.

# Niwahakikishie wakulima kuwa hadi kufikia Septemba 30, 2019, Serikali imeshauza korosho zote kwa jumla ya wanunuzi 21 wa ndani na nje ya nchi. Kuna tani zaidi ya 4,595.90 zitabanguliwa nchini na zaidi ya tani 211, 587 ambapo tani 107,187 zitapitia Bandari ya Dar na tani 104,400 kupitia Bandari ya Mtwara zitasafirishwa kwenda nje ya Tanzania.

# Hadi sasa zaidi ya tani 98,860 zimekwishachukuliwa na kusafirishwa nje ya nchi kupitia Bandari za Mtwara na Dar sawa na asilimia 41 ya korosho zote na zoezi la kuondoa korosho iliyobaki kupelekwa kwa wanunuzi linatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 21 mwaka huu”

# Naomba kusisitiza tena, faida kubwa ya mchakato huu ni kwa wakulima kupata bei ya haki katika zao la korosho lakini funzo la korosho si tu limeweka mazingira mazuri zaidi katika misimu ijayo ambapo korosho itanunuliwa kwa mfumo madhubuti lakini pia mazao mengine yamepata nguvu ya kuwekewa mifumo na hivyo wakulima kupata bei inayowanufaisha kwa kuwapa faida.

# Kati ya Julai na Septemba, 2019, jumla ya TZS Bilioni 85.72 zimetolewa ikiwemo Bilioni 50 za madai ya pensheni; Bilioni 22 madai ya watumishi wa umma ikiwemo kiinua mgongo kwa wastaafu 3,019 na malimbikizo ya mishahara kwa watumishi 1,435; Bilioni 10.24 zimelipa watoa huduma mbalimbali na zaidi ya Bilioni 2 kwa ajili ya wakandarasi na waandishi washauri

Updated: 03.10.2019 16:51
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.