Aliwa na mamba wakati akifanya tukio la kiimani ziwani

Ni mchungaji aliyekuwa akibatiza watu

Aliwa na mamba wakati akifanya tukio la kiimani ziwani

Ni mchungaji aliyekuwa akibatiza watu

06 June 2018 Wednesday 11:38
Aliwa na mamba wakati akifanya tukio la kiimani ziwani

MTU mmoja ameuawa na mamba alipokuwa anafanya mambo ya kiimani ya dini ya kikristo kwenye mto mmoja nchini Ethiopia.

Taarifa zinasema kuwa Mchungaji wa Kiprotestanti Docho Eshete aliyekuwa akibatiza watu katika ziwa Ayaba kusini mwa Ethiopia ameliwa na mamba.

Mashambulizi yaliyo karibu na mji wa Arba Minch yanahusishwa na kupungua idadi ya samaki ambacho ni chakula cha Mamba na hivyo kuanza kuvamia watu na kuwaua.

Mchungaji, Docho, ndiyo kwanza alikuwa ameanza kumbatiza mfuasi wa kwanza kati ya themanini waliokwenda kufanyiwa huduma hiyo katika ziwa Ayaba, huko Ethiopia wakati mamba aliporuka nje kutoka majini na kumchukua mchungaji huyo.

Mchungaji alijitahidi kupambana na kujiokoa na mashambulizi ya mamba huyo ambaye alikuwa amemsababishia majeraha makubwa.

Wakazi wa eneo hilo ikiwa ni pamoja na wavuvi walijaribu kutumia nyavu ili kumuokoa na mamba huyo asimwingize kwenye kina kirefu ndani ya ziwa hilo lakini hata hivyo juhudi zao hazikuweza kuokoa maisha ya mchungaji huyo na walichoweza ni kuopoa mwili wake baada ya kuwa tayari amefariki.

Watu wanaoishi karibu na ziwa hilo katika mji wa Arba Minch wanasema uvuvi uliopindukia umesababisha kupungua kwa chakula cha mamba na matokeo yake mamba wamekuwa wakionekana wakiwinda kando kando ya ziwa.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.