banner68

Aliyedai kutelekezwa na Lowassa aomba radhi

Nilikuwa naomba radhi kwa kilichotokea mitandaoni

Aliyedai kutelekezwa na Lowassa aomba radhi

Nilikuwa naomba radhi kwa kilichotokea mitandaoni

16 April 2018 Monday 16:51
Aliyedai kutelekezwa na Lowassa aomba radhi

Mkazi wa Kigamboni Fatuma Selemani Chikawe amemuomba radhi Waziri Mkuu wa zamani na mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa kufuatia kashfa aliyomzushia akidai kuwa ni baba yake.

Mwanamke huyo ameomba radhi na kujutia alichokifanya kwani hakutegemea kama mambo yangefikia hapo ambavyo watu wameichukulia kisiasa, amedai kuwa ni siku nyingi amekuwa akimtafuta Lowassa ili amsaidie ila jitihada hizo ziligonga mwamba ndipo alipoamua kutumia njia hiyo.

”Nilikuwa naomba radhi kwa kilichotokea mitandaoni ambapo nimemdhalilisha mzee ambaye ni Edward Lowassa mtandaoni, lakini sikutegemea kama ingekua vile.

“Nilienda vile kama kuomba msaada anisaidie sababu miaka mingi namtafuta mzee, lakini kilichotokea hata mimi nafsi yangu inaniuma na sikutegemea kama ingekuwa vile sina amani, kwenye familia yangu, mtaani najuta sababu najua huyo mzee nimemkwaza kwa kiasi fulani sababu yeye ana familia yake ana watoto wake, sijajua wamelipokea vipi.

“Pia hilo linaniuma na mzee kama yule kumuweka kwenye mitandao roho inaniuma kwahiyo naomba aniwie radhi anisamehe kwa kilichotokea.

“Mambo yametumika kisiasa, nashambuliwa na maneno sina amani na maisha yangu na familia yangu,” amesema Fatma.

Kufuatia zoezi linaloendelea jijini Dar es salaam, ambapo Mkuu wa Mkoa wa huo, Paul Makonda ameamua kuwasaidia kisheria wanawake waliozalishwa na kutelekezwa, Fatma alijitokeza akidai kuwa baba yake ni Edward Lowassa na ameanza kumtafuta tangu akiwa darasa la sita bila mafanikio.

Hata hivyo Lowassa alihojiwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini kufuatia kashfa hiyo alikanusha kuhusika na mtoto huyo na alidai kuwa hata kupima DNA ”vina saba” ni upuuzi.

Dar24

Updated: 16.04.2018 17:01
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.