Aliyempiga makofi rais Mwinyi azikwa

"Alifanya tukio hilo Machi 10, 2009 wakati Mwinyi alikuwa akihutubia katika sherehe za Maulidi zilizofanyika Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam"

Aliyempiga makofi rais Mwinyi azikwa

"Alifanya tukio hilo Machi 10, 2009 wakati Mwinyi alikuwa akihutubia katika sherehe za Maulidi zilizofanyika Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam"

03 June 2019 Monday 10:22
Aliyempiga makofi rais Mwinyi azikwa


Na mwandishi wetu, Dar es Salaam 

 KIJANA Ibrahim Said maarufu Sultan mkazi wa Mabibo Loyola ambaye alimpiga makofi rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi amefariki dunia asubuhi  ya Juni 2, 2019 na kuzikwa mchana wake.

Marehemu alijipatia umaarufu kutokana na kitendo chake cha kumchapa kibao mzee Mwinyi akimtuhumu kitendo cha kuhimiza  matumizi ya kondomu ambayo ni kinyume na imani ya Kiislamu

Alifanya tukio hilo Machi 10, 2009 wakati Mwinyi alikuwa akihutubia katika sherehe za Maulidi zilizofanyika Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lilikuwa la  kushtukiza kwani kila mtu alidhani kijana huyo alikuwa anakwenda kumsalimia Kaimu Mufti alimaruhumu Sheikh Suleyman Gorogosi aliyekuwa pembeni ya Mzee Mwinyi.


Wengine walidhani kijana ni fundi mitambo na hivyo alikuwa anakwenda kurekebisha kipaza sauti.


Tofauti na mawazo ya wengi,kijana huyo aligeuza mkono ghafla na kumnasa kibao Mzee Mwinyi.


Wakati huo alikuwa na umri wa miaka  26.


Kabla ya kitendo hicho,Mzee Mwinyi,kama ambavyo amekuwa akifanya mara kwa mara,alikuwa akiwaasa waliohudhuria baraza hilo la Maulid kuepukana na ngono zembe kitu ambacho kinachangia sana kuenea kwa ugonjwa wa ukimwi.


Alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela lakini hakumaliza kifungo aliachiwa kwa msamaha wa rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete

Updated: 03.06.2019 20:12
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Lucas peter 2019-07-03 21:59:11

R I P