Amuua kaka yake ahukumiwa miaka mitatu jela

Amuua kaka yake ahukumiwa miaka mitatu jela

12 July 2019 Friday 06:34
Amuua kaka yake ahukumiwa miaka mitatu jela

Na mwandishi wetu, Dar es Salaa,

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imemuhukumu kifungo cha miaka mitatu jela Rukia Ally baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kaka yake Said Ally bila ya kukusudia.

Hukumu hiyo ilitolewa lJulai 11,2019 na msajili wa mahakama hiyo Pamela Mazengo baada mshtakiwa huyo kukiri kosa la kumuua Said bila ya kukusudia ndipo mahakama hiyo imemkuta na hatia hiyo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi,Mwasiti Ally alipomsomea mshtakiwa huyo kosa lake alikiri kuua bila ya kukusudia.

Mwasiti alidai kuwa mshtakiwa huyo na marehemu Said ni ndugu wa damu walikuwa wanaishi na wazazi wao maeneo ya Mivumon Madale

Alidai kuwa sikuya tukio majira ya jioni marehemu alirudi nyumbani na kumkuta Rukia ambaye aliondoka siku tatu bila ya kuonekana hivyo siku hiyo alikuwa amerudi nyumbani hapo.

Marehemu aligonga chumbani kwake na kumuuliza siku zote ulikuwa wapi lakini Rukia hakumjibu kitu hivyo marehemu akaanza kumchapa kwa fimbo miguuni .

Wakati tukio linatokea marehemu alikuwa na kisu ndipo Rukia akampokonya kisu hicho kwa bahati mbaya alimchoma kwenye kifua kushoto ndipo Said alianguka na kutokwa na damu nyingi.

Hakimu Mazengo alisema mshtakiwa amekiri kosa lake ambalo limesababisha mauaji ya kutokusudia kwa kumuua kaka yake Said hivyo mahakama hiyo imeona mshtakiwa ana hatia ya kuua .

Wakili wa Utetezi,Musa Mhagama aliiomba mahakama hiyo kutumia mamlaka yake itumie kifungo cha 38 kifungo kidogo cha kwanza cha sheria kanuni ya adhabu sura ya 16 ya mwaka 2002.

"Namna kosa liiivyotendeka mshtakiwa aliweza kutenda kosa baada ya marehemu kushika kisu lakini wakati huo wote wawili hawakuwa na mahusiano mazuri,"alidai wakili huyo

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.