Askari sita kizimbani wakituhumiwa kwa wizi wa mafuta ya ndege

Askari sita kizimbani wakituhumiwa kwa wizi wa mafuta ya ndege

11 September 2019 Wednesday 06:43
Askari sita kizimbani wakituhumiwa kwa wizi wa mafuta ya ndege

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

ASKARI Polisi watano na Mwanajeshi mmoja wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo wizi wa mafuta ya ndege na Utakatishaji wa fefha zaidi ya milioni 4.6

Washtakiwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 93/2019 ni Koplo Shwahiba (38), MT. 74164 SGT Ally Chibwana (47), wa jeshi la wananchi Tanzania, PC Elidaima Paranjo (38), PC Simon (28), PC Dickson na PC Hamza.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi, Vicky Mwaikambo, Wakili wa serikali Faraji Nguka akisaidiana na Saada Mohammed alidai washtakiwa wote wakiwa ni watumishi wa umma walikiuka maadili ya kazi zao na kupanga genge la uhalifu na kuiba lita 2180 za mafuta ya ndege( Jet A-1/Ik yenye thamani ya sh. 4,647,760.

Katika shtaka la pili inadaiwa, Julai 30,2019 katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere Wilayani Ilala jijini Dar ea Salaam, watuhumiwa hao(askari), waliiba lita 2180 za mafuta ya ndege aina ya (Jet A-1/Ik yenye thamani ya sh. 4,647,760 mali ya shirika la ndege Tanzania ATCL

Katika shtaka la tatu imedaiwa, siku na eneo hilohilo washtakiwa wote kwa pamoja walifanya wizi wa mafuta hayo na kutakatisha fedha kiasi cha shilingi 4.6 milioni ambapo wakijua fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la wizi kinyume na Sheria.

Hata hivyo,baada ya kusomewa mashtaka hayo hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. Watuhumiwa wamerudishwa rumande hadi Septemba 24, 2019 kesi hiyo itakapokuja kutajwa.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.