Askofu Ruwaichi Kardinali mpya Dar es Salaam

Askofu Ruwaichi Kardinali mpya Dar es Salaam

15 August 2019 Thursday 14:50
Askofu Ruwaichi  Kardinali  mpya  Dar es Salaam

Vatican, Italia

BABA Mtakatifu Francis amemteua Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza Yuda Thaddeus Ruwaichi kuwa mrithi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, ambalo limekuwa linaongozwa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Padri Richard A. Mjigwa wa Vatican News ameandika katika mtandao wa Vatican, na Padri Raymond Saba, Katibu Mkuu wa Baraza la Maskofu Tanzania (TEC) ametoa taarifa rasmi kwa umma kuhusu uteuzi huo.

Kwa uteuzi huu maana yake ni kwamba mchakato wa kustaafu kwa Kardinali Pengo umekamilika, hasa kutokana na matakwa ya kisheria kuhusu umri, na kwa sababu ya afya yake kutetereka. Kardinali Pengo atastaafu rasmi mwakani (2019) atakapotimiza umri wa miaka 75.

Kabla ya kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Pengo naye aliteuliwa kuwa askofu Mkuu Mwandamizi Mwenye Haki ya Kurithi Januari 22, 1990. Aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Julai 22 1992 baada ya kustaafu kwa Mwadhama Laurean Kardinali Rugambwa.

Kabla ya uteuzi huu, Askofu Mkuu Ruwaichi alikuwa ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza tangu Novemba 10, 2010. Kwa uteuzi huu wa leo, Askofu Mkuu Ruwaichi amepitia katika mikono ya wateuzi watatu – Papa Yohanne Paulo II, Papa Benedicto XVI, na Papa Francis.

Askofu Mkuu Ruwaichi alizaliwa Januari 30, 1954, Mulo, Kilema, Jimbo Katoliki la Moshi. Alipadirishwa Novemba 25, 1981, akapewa daraja la uaskofu Februari 9, 1999, kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Mbulu, na akawekewa wakfu Mei 16, 1999.

Januari 15, 2005, Baba Mtakatifu Yohane Paulo II akamteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Dodoma na kusimikwa rasmi tarehe 19 Februari 2005.

Novemba 10, 2010, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteua kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza, akasimikwa rasmi tarehe 9 Januari 2011.

Updated: 15.08.2019 15:09
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.