Bunge kuomboleza kifo cha Mbunge Chadema kwa siku mbili

Mwili wa mbunge huyo unatarajiwa kuagwa kesho mchana, bungeni Dodoma

Bunge kuomboleza kifo cha Mbunge Chadema kwa siku mbili

Mwili wa mbunge huyo unatarajiwa kuagwa kesho mchana, bungeni Dodoma

28 May 2018 Monday 11:41
Bunge kuomboleza kifo cha Mbunge Chadema kwa siku mbili

Na Mwandishi Wetu

BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litaomboleza kifo cha Mbunge wa Buyungu, Kasuku Bilago (chadema) kwa muda wa siku mbili, hadi Jumatano.

Akisoma taarifa ya Spika leo bungeni, Naibu Spika Tulia Ackson alisema kuwa mwili wa mbunge huyo aliyefariki jana katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili unatarajiwa kupelekwa bungeni kesho mchana kwa ajili ya kuuga.

Alisema baada ya kuuaga mwili huo, Bunge litaahirisha kikao chake kwa ajili ya kuomboleza hadi siku ya Jumatano ambapo litaendelea kama kawaida.

Kwa mujibu wa kanuni 33 (2) ya mwaka 2006 ya Bunge la Jamhuri ya Muungano leo hakutakuwepo na kikao cha bunge, badala yake wabunge watakuwa wanaomboleza kifo cha mwenzao.

Aliongeza kuwa mwili wa Bilago utasafirishwa kesho mchana kuelekea kijiji cha Kasuga wilayani Kakonko kwa mazishi siku ya Jumatano.

Azania Post

Updated: 28.05.2018 12:15
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.