banner58

CRDB yafunga tawi lake kwa sababu za kiusalama, Mbunge adai

CRDB yafunga tawi lake kwa sababu za kiusalama, Mbunge adai

29 May 2018 Tuesday 11:47
CRDB yafunga tawi lake kwa sababu za kiusalama, Mbunge adai

Na Mwandishi Wetu

TAWI la benki ya CRDB lililopo maeneo ya Chanika wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam limefungwa kwa sababu za kiusalama, Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara (Chadema) amesema.

Mbunge huyo alikuwa akiuliza swali la nyongeza alisema kuwa eneo la Chanika halina gari la polisi la patrol na idadi ya wananchi inaongezeka na uhalifu pia

Alisema kuwa gari iliyopo kwa sasa inatumika na OCS na kuwa tawi la benki ya CRDB limefungwa kwa sababu za kiusalama alitaka kujua mpango wa haraka kukisaidia kituo hicho kikubwa cha polisi usafiri.

Akijibu swali hilo Naibu waziri wa Mambo ya ndani, Hamad Masauni, alisema kuwa serikali kupitia jeshi la polisi itaangalia uwezekano wa kuongeza gari la patrol kwa kituo hicho baada ya kuzingatia vigezo

Alisema kuwa vigezo hivyo ni pamoja na upatikanaji wa fedha, idadi ya wakazi na kiwango cha uhalifu katika eneo husika.

Aliongeza kuwa anatambua juhudi za Mbunge huyo katika kuhakikisha kuwa maeneo yote yanakuwa salama na akaahidi kwenda kufanya harambe kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha polisi kule Kivule.

Hata hivyo naibu waziri huyo alisema kuwa serikali inatambua changamoto za magari ya polisi katika maeneo mengo na itaangalia uwezekano wa kuyafanyia ukarabati yale yaliyopo.

Baadhi ya maeneo majimbo ambayo wabunge wake wamelalamika upungufu wa magari ni pamoja na Arusha na Kivuu na huko Kisiwani Pemba.

Kuhusu Pemba, Naibu waziri huyo alisema kuwa ni kweli kituo cha polisi Konde kimechakaa ikiwa ni pamoja na nyumba za walinda usalama hao

Aliwataka wabunge husika kuangalia uwezekano wa kutumia fedha za mfuko wa jimbo katika kununua vitu vidogo kama mabati na mifuko ya saruji badala ya kuisubiri serikali.

Alidokeza kuwa katika kukabiliana na upungufu wa watenda kazi, serikali imetoa kibali cha kuajiri askari wapatao 1500 nchi nzima mwaka huu.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.