Diamond balozi wa vvu nchini

Diamond balozi wa vvu nchini

11 July 2019 Thursday 08:53
Diamond balozi wa vvu nchini

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

TUME ya kudhibiti Ukimwi nchini(TACAIDS) imemteua mwanamuziki Diamond Platinumz kuwa balozi wa kukabiliana na maambukizi ya virusi kwa ukimwi(VVU).

Siku tatu baada ya kufanyika kwa sherehe ya siku ya kuzaliwa na tangazo lake rasmi kwamba mpenzi wake kutoka Kenya Tanasha Donna alikuwa ni mjamzito wa mtoto wake wa nne, 

Hatua hiyo imetangazwa Julai 10, 2019 na  TACAIDS  baada ya kufikia makubaliano  na msanii huyo wa Wasafi Records .

Kaimu mkurugenzi wa tume hiyo, Jummanne Issango amesema  mkakati wa nne wa kuangamiza Ukimwi umejikita kuwahamasisha vijana kuhusu afya ya uzazi pamoja na kutoa hamasa kuhusu ugonjwa huo.

Akizungumza baada ya uteuzi wake Diamond Platinumz alisema kwamba iwapo wanawake wangekataa katakata kuwaruhusu wanaume kushiriki tendo la ngono bila kinga basi hatua hiyo ingepunguza maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi nchini.

''Ninaamini kwamba iwapo wanawake watatilia mkazo swala la hakuna ngono bila kinga wanaume watalazimika kutumia kinga''.

Akizungumzia kuhusu ushirikiano wa kufanya kazi na TACAIDS kupitia tamasha la Wasafi, Diamond amesema  kampeni hiyo imejiri wakati mzuri kwa kuwa tamasha hilo sio tu kuhusu burudani bali pia kutoa elimu kwa vijana.

Afisa wa baraza la sanaa nchini (Basata) aliunga mkono hatua hiyo ya TACAIDS akisema kuwa walifanya uamuzi mzuri kuwatumia wasanii kutokana na ushawishi walio nao miongoni mwa Vijana kupitia mitandao ya kijamii.

Tamasha hilo la Wasafi linatarajiwa kuanza Julai 19 2019.

Updated: 11.07.2019 09:05
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.