Erick Kabendera kujadiliana na DPP

Erick Kabendera kujadiliana na DPP

11 October 2019 Friday 16:51
Erick Kabendera kujadiliana na DPP

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.

WAKILI wa Erick Kabendera, Jebra Kambole ameijulisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa, Kabendera anakusudia kuanza majadiliano na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ya namna ya kumaliza kesi inayomkabili.

Kambole ameeleza hay oleo Oktoba 11, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.

Awali wakili wa Serikali ,Wankyo Simon alidai kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika.

Baada ya Wankyo kueleza hayo, Wakili wa utetezi Kambole aliijulisha Mahakama taarifa hiyo kwa mujibu wa kifungu namba 194A(2) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

Baada ya Kambole kueleza hayo,Wakili wa Serikali,Wankyo Simon aliieleza Mahakama kuwa ni kweli jambo hilo limefanyika.

Na kubainisha kuwa Kabendera ameandika barua na kwamba ipo Katika mchakato na kwamba watakapokuwa wamekamilisha wataitaalifu Mahakama.

Hata hivyo baada ya kusikiliza hoja hizo Hakimu Rwizile aliiahirisha Kesi hiyo hadi Oktoba 24, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa. Na kama kutakuwa na chochote kabla ya hiyo tarehe waiharifu Mahakama.

Kabendera ambaye ni mwandishi wa habari, anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya milioni 173.

Katika shtaka la kwanza ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Shtaka la pili ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho,bila ya sababu,alikwepa kodi ya sh. 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika shtaka la tatu, kabendera anadaiwa kutakaisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na utakatishaji fedha.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.