Facebook yafuta akaunti bilioni 3

"Kampuni hiyo ilizindua mradi wa kuangalia uhakika wa taarifa mnamo 2016 muda mfupi baada ya rais Trump wa Marekani kuingia madarakani"

Facebook yafuta akaunti bilioni 3

"Kampuni hiyo ilizindua mradi wa kuangalia uhakika wa taarifa mnamo 2016 muda mfupi baada ya rais Trump wa Marekani kuingia madarakani"

24 May 2019 Friday 09:26
Facebook yafuta akaunti bilioni 3

MTANDAO wa Facebook imefunga zaidi ya akaunti bilioni tatu feki, idadi ambayo inasema ni kubwa zaidi kuwahi kufungwa.

Akaunti feki hizo zilizochukuliwa hatua kati ya mwezi Oktoba 2018 na Machi 2019.

Katika kipindi hicho cha miezi sita, zaidi ya ujumbe milioni saba za"chuki" pia zilitolewa katika mtandao huo wa kijami.

Kwa mara ya kwanza, Facebook pia iliripoti kuwa baadhi ya watumiaji wa mtandao huo ambao ujumbe wao ulifutwa wamekata rufaa na kuongeza kuwa zingine zilirudishwa baada ya uchunguzi wa kina.

Akizungumza na vyombo vya habari mwanzilishi wa mtandao huo Mark Zuckerberg aliwakosoa vikali wale ambao wanatoa wito kampuni hiyo ivunjiliwe mbali, akiongeza kuwa wanafanya kila wawezalo kukabiliana na changamoto zinazoibuka.

"Sidhani suluhisho ni kuvunjilia mbali kampuni kwasababu tunashughulikia [tatizo hilo]," alisema.

"Ufanisi wa kampuni hii umetuwezesha kufadhili mpango huu kwa kiwango kikubwa. Kiwango cha fedha tunazotumia kuimarisha usalama wa mtandao wetu ni kikubwa kuliko ''mapato ya mwaka mzima'' ya mtandao wa Twiter.

Facebook imesema kumekuwa na ongezeko la akaunti bandia kwasababu "wahalifu" wamekuwa wakitumia mfumo maalum kuzifungua.

Lakini ikaongeza kuwa ilifanikiwa kuzigundua na kuzifuta zote katika kipindi cha dakika moja, kabla awajapata nafasi ya kuzitumia kufanya "uhalifu ".

Mtando huo wa kijamii pia utaripoti ni posti zilizotolewa kwa kuuza "bidhaa ambazo zimedhibitiwa"kama vile bunduki na dawa.

Ilisema kuwa iliwachukilia hatua watumiaji milioni moja wa mtandao huo kwa kuuza bunduki katika miezi hiyo sita kipindi ambacho ilichukua kuaanda ripoti hiyo.

Ripoti hiyo pia ilikadiria idadi ya ujumbe, kama zile zinazoangazia unyanyasaji watoto, ghasia na propaganda kuhusu ugaidii,zinazowafikia wateja wake.

Uchunguzi huo ulibaini ni mara ngapi posti 10,000 zilizo na ujumbe huo zilionekana kwenye Facebook:

Watu wachache kati 14 waliona picha za utupu

Karibu watu 25 waliona taarifa zilizo na ujumbe wa kuchochea ghasia

Wachache kati ya watu watatu waliona taarifa zilizo na ujumbe wa unyanyasaji wa watoto na propaganda kuhusu masuala ya ugaidi
Kwa ujumla, karibu ya 5% ya watumiaji wa mtandao huo wanafanya hivyo kupitia akaunti feki.

Kwa mara ya kwanza, ripoti hiyo ilifichua kuwa kati ya mwezi Januari na Machi 2019 zaidi ya watumiaji milioni moja wa mtandao huo walikata rufaa baada ya akaunti zao kufungiwa kwa kuposti ujumbe uliyo na ''kauli za chuki".

Karibu watumiaji 150,000 walifunguliwa akaunti zao baada ya kubainika kuwa hawakukiuka sheria kipindi hicho.

Facebook imesema ripoti hiyo imeangazia masuala hayo ili kuendesha huduma zake kwa njia ya uwazi na uwajibikaji ili kuufanya mtandao huo kuwa ''salama kwa wateja wake".

Hivi karibuni Facebook iliondosha mamia ya akaunti za mitandao ya kijamii na kupiga marufuku kampuni ya Israel kutokana na inachotaja kuwa "Tabia za uongo zilizoratibiwa" zinazoilenga Afrika.

Akaunti hizo bandia mara nyingi huweka taarifa za kisiasa, ikiwemo uchaguzi katika baadhi ya mataifa , kampuni hiyo  imekabiliwa na shutuma kwa kushindwa kudhibiti taarifa za uongo katika jukwaa hilo la mtandao wa kijamii.

Kampuni hiyo ilizindua mradi wa kuangalia uhakika wa taarifa mnamo 2016 muda mfupi baada ya rais Trump wa Marekani kuingia madarakani .

Katika ujumbe kwenye blogu, Facebook ilisema imeondosha akaunti 265 za mtandao wa kijamii zilizofunguliwa nchini Israel na zilizoilenga Nigeria, Senegal, Togo, Angola, Niger na Tunisia, pamoja na kushuhudiwa "sehemu ya shughuli zake" Amerika kusini na Kuisni mashariki mwa Asia.

Walikuwa na majina kama 'Hidden Africa' na siri ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Ujumbe huo ulionekana kumuunga mkono rais mpya wa Felix Tshisekedi na kumuomba mgombea wa upinzani akubali kushindwa.

"Watu wanaohusika na mtandao huu walitumia akaunti bandia kuendesha kurasa hizo, kusambaza taarifa zao na kuongeza mawasiliano kwa njia za uongo.

"Walijifanya kuwa watu kutoka mataifa hayo, wakiwemo kutoka vyombo vya habari nchini, na kuchapisha na kutuhumiwa kufichua taarifa kuhusu wanasiasa" Nathaniel Gleicher, mkuu a kitengo cha kupambana uhalifu wa mtandaoni katika Facebook, ameandika katika ujumbe huo.

Uchunguzi huo ulibaini kwamba shughuli hizo zimehusishwa na kampuni ya Israeli - Archimedes Group, Gleicher ameongeza.

"Shirika hilo na matawi yake sasa yalipigwa marufuku kutoka Facebook, na kupewa onyo kali la kusitisha shughuli hizo," alisema.

Wahusika wa akaunti hizo walitumia $812,000 kwa matangazo kati ya Disemba 2012 na April 2019, Facebook imesema, na fedha hizo zimelipwa kwa kutumia sarafu ya Brazilian reais, ya Israeli shekel na dola za Marekani.

BBC

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.