banner68
banner58

Gari la mbunge Chadema lashambuliwa kwa risasi Monduli

Gari la mbunge Chadema lashambuliwa kwa risasi Monduli

16 September 2018 Sunday 16:49
Gari la mbunge Chadema lashambuliwa kwa risasi Monduli

ANNA Gidarya, Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Manyara ameeleza kuwa, gari lake limeshambuliwa kwa risasi leo tarehe 16 Septemba 2018.

Anna amesema, risasi hizi zimepiga kwenye matari yake ya gari na Sasa anaelekea katika Kituo cha Polisi cha Mto wa Mbu kutoa maelezo.

Anaeleza kuwa, shambulizi hilo limetokea katika Kata ya Majengo, wilayani Monduli katika Mkoa wa Arusha.

Mbunge huyo anaeleza kuwa, yupo Monduli kusimamia na kufuatilia uchaguzi wa ubunge kwenye Jimbo la Monduli leo.

Updated: 16.09.2018 16:54
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.