Gari la naibu waziri lapata ajali, watano wafariki dunia

Gari la naibu waziri lapata ajali, watano wafariki dunia

12 September 2019 Thursday 14:00
Gari la naibu waziri lapata ajali, watano wafariki dunia

Na Ashiraki Miraji, Mombo

TAKRIBANI watu watano wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea kijiji cha Kasiga Mombo wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Ajali hiyo imetokea Septemba 11, 2019 majira ya saa moja na nusu usiku baada gari aina ya Land Cruiser Prado lililokuwa na namba NW (Naibu Waziri Ofisi Ya Makamu Wa Rais Muungano ) likitokea Moshi kugongana uso kwa uso na Noah.

Noah hiyo inayofanya safari kati ya Mombo na Hedaru ilikuwa na abiria 15 huku gari hilo la Naibu Waziri likiwa na watu wanne(Wanawake wawili na mtoto mmoja)

Waliofariki ni abiria wanne na dereva wa Noah huku dereva wa Naibu Waziri   amevunjika mguu wa kushoto.

Daktari wa hospitali ya kata ya Mombo(jina tunaliifadhi) ameiambia Azaniapost kuwa walipokea miili mitano ikiwa imefariki papo hapo na kwamba waliisafirisha kwenda hospitali ya wilaya ya Korongwe.

‘‘Kunako majira ya saa mbili usiku tulipokea miili mitano ikiwa imeshafariki na majeruhiwa lakini kutokana na kutokuwa na majokofu ya kuhifadhi maiti tuliiamishia katika hospitali ya wilaya ya Korogwe,’’ amesema dokta huyo na kuongezea

‘‘Dereva wa naibu waziri alivunjika mguu wa kushoto na majeruhi wengine nao kwa pamoja baada ya kuwapa huduma ya kwanza tuliwahamishia hospitali ya wilaya ya Korogwe’’

Shuhuda mmoja amesema ajali hiyo ilisabishwa na dereva wa Noah ambaye alikuwa akilipita(Overtake) lori na ndipo gari lilimshinda na kuelekea upande wa lilipokuwa gari hilo la Naibu Waziri Ofisi Ya Makamu Wa Rais Muungano Na Mazingira, Mussa Sima

Updated: 12.09.2019 19:26
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.