Gawio kwa serikali, TTCL yajikongoja

"TTCL iliahidi kutoa gawio kubwa zaidi kwa serikali, fedha hizo zikasaidie kazi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege vya serikali"

Gawio kwa serikali, TTCL yajikongoja

"TTCL iliahidi kutoa gawio kubwa zaidi kwa serikali, fedha hizo zikasaidie kazi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege vya serikali"

21 May 2019 Tuesday 14:45
Gawio kwa serikali, TTCL yajikongoja

Na mwandishi wetu, Dar es salaam
SHIRIKA la Mawasiliano nchini (TTCL), limeongeza milioni 600 katika gawio lake kwa serikali  kutoka bilioni 1.5 mwaka 2018 hadi bilioni 2.1 mwaka 2019.

Mwaka jana (2018) TTCL kupitia Mkurugenzi Mkuu wake,  Waziri Kindamba aliahidi kutoa gawio kubwa zaidi kwa serikali ili fedha hizo zikasaidie katika kazi mbalimbali ukiwemo ujenzi wa miundombinu ya viwanja vya ndege vya serikali.

Kindamba alitoa ahadi hiyo Agosti 6, 2018 Mkoani Simiyu alipokuwa ametembelea banda la maonesho ya Kilimo la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), yaliyofanyika Uwanja wa Nyakabindi mkoani Simiyu.

Alisema wingi huo wa fedha utatokana na mashirika na taasisi za umma kuwaunga mkono kwa kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo.

Gawio la  bilioni 2.1 limetangazwa na Kindamba hii leo Mei 21, 2019 jijini Dar es salaam katika hafla  iliyoudhuliwa na rais Dk John Magufuli, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Omar Nundu huku Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki kwa njia ya Teknolojia ya mawasiliano ya video moja kwa  moja Kutoka Dodoma.

 Kindamba amesema makubwa yalianza kuonekana kupitia uongozi wa awamu ya tano na kwamba mwaka uliopita mapato yalikuwa bilioni 119 na mwaka huu ni bilioni 167


Kindamba ameongeze kuwa katika juhudi za kuimarisha shirika hilo, wameendelea kutekeleza maagizo ya serikali baada ya kupunguza safari za nje kwa watendaji wake na kufuta mikataba mibovu isiyokuwa na manufaa kwa shirika.

Aidha Rais Magufuli amelitaka Shirika hilo kuhakikisha linakusanya vyema madeni kwa wateja wake na kwa mafanikio hayo makubwa waliyoyapata ameamuru wafanyakazi kupandishiwa mishahara.

Updated: 22.05.2019 04:58
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.