banner68

Gharama za ujenzi wa barabara kiwango cha lami zaitisha serikali

Gharama za ujenzi wa barabara kiwango cha lami zaitisha serikali

11 June 2018 Monday 15:08
Gharama za ujenzi wa barabara kiwango cha lami zaitisha serikali

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema kuwa itapitia upya gharama za ujenzi wa barabara kiwango cha lami na kuona kinapungua ili kubana matumizi kwa ajili ya shughuli nyingine.

Hayo yameelezwa bungeni leo na Naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ilala Musa Azan Zungu (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua ni lini serikali itapitia upya gharama za ujenzi wa barabara kiwango cha lami.

Alisema kuwa gharama hizo ni kubwa mno kwani hata maeneo ya mjini kilomita moja inagharimu shilingi bilioni 1.4

“Ujenzi huo wa mjini utakuta hakuna daraja wala kalavati, lini serikali ita revisit gharama ili kusave pesa?” alihoji.

Akijibu, Naibu waziri Kwandikwa alisema kuwa ni kweli gharama ni kubwa sana na serikali imechukua hatua ya kufanyia mapitio kupunguza gharama.

Alisema kuwa gharama hizo zinapanda kutokana na riba, bei ya vifaa, teknolojia na  usimamizi wa mradi husika.

Alisema wataliagiza baraza la ujenzi la taifa lije na utaratibu wa kutazama gharama za ujenzi.

Aliongeza kuwa wataangalia makandarasi na kutumia teknolojia  ya kisasa katika ujenzi kwa lengo la kupunguza gharama.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.