Hakimu awataka wananchi wasiikimbie Mahakama Mtaani

Hakimu awataka wananchi wasiikimbie Mahakama Mtaani

12 September 2019 Thursday 19:10
Hakimu awataka wananchi wasiikimbie Mahakama Mtaani

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Ukonga, Faudhia Hamza amewataka wananchi wasiikimbie Mahakama inayotembea maarufu ‘Mahakama Mtaani’ na wajitokeze kutoa dukuduku, malalamiko na vinyongo vyao.

Ametoa wito huo leo Septemba 12,2019 wakati akiendesha mahakama hiyo eneo la Chanika wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.

"Wananchi nawaomba mnapoliona hili gari la mahakama inayotembea msilikimbie wala kufikiri kuwa sasa mtafungwa , huu ni ukombozi wenu jitokezeni ili kutatua matatizo hasa yanayohusiana na madai, mirathi na ndoa," amesema Hakimu Hamza na kuongeza.

‘‘Katika jamii, watu wanakaa na mambo moyoni na kupelekea kuchukua maamuzi magumu ikiwamo kujinyonga kutokana na kukosa ushauri ama elimu’’

‘‘Hivyo mahakama hii inayotembea ipo kwa ajili ya wananchi inapokea kesi ikiwemo vinyongo, madukuduku na malalamiko mlivyonayo wananchi na kuwashauri kwa mujibu wa sheria na taratibu zake.’’

Naye Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Martha Mpaze amesema mahakama hiyo inayotembea imejikita kusikiliza kesi za madai, talaka na Mirathi kwa kutoa usuluhishi zaidi na kwamba maamuzi yanatolewa ndani ya siku 30.

Amesema wamesogeza huduma hizo karibu na wananchi ili kuhakikisha haki inatendeka kwa usawa, urahisi na kwa wakati.

Mkazi wa Chanika ambaye pia ni Katibu wa CCM, Yahya Rajabu ameshukuru Mahakama kwa kusogeza mahakama mtaani.

Amesema itasaidi wananchi kupata uelewa wa sheria kwa kuwa wengi wanakabiliwa na changamoto ya migogoro katika talaka.

Huduma ya mahakama inayotembea ‘mahakama mtaani’ imeanza kazi mwaka huu na kwa sasa inafanyakazi katika Mkoa wa Dar es Salaam na Mwanza.

PICHANI:Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Ilala, Martha Mpanze akizungumza na katibu wa CCM Chanika, Yahya Rajabu na mwenzake kuhusu mahakama  inayotembea na  kila siku ya Alhamisi  itakuwepo Chanika katika ofisi za serikali ya mtaa huo

Updated: 13.09.2019 06:47
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.