Idadi waliofariki ajali ya moto Morogoro yafikia 82

Idadi waliofariki ajali ya moto Morogoro yafikia 82

14 August 2019 Wednesday 15:22
Idadi waliofariki ajali ya moto Morogoro yafikia 82

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

AJALI ya mlipuko wa lori la mafuta mjini Morogoro inaendelea kugharimu maisha ya watu na hivi sasa waliofariki kutokana na mkasa huo wa Agosti 10, 2019 imefikia 82.

Idadi hiyo imeongezeka baada ya majeruhi sita kati ya wale 38 waliolazwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) kuaga dunia,

Watu 62 walithibitishwa kufariki siku ya mkasa na zaidi ya 70 kujeruhiwa, na toka hapo idadi ya vifo imekuwa ikiongezeka taratibu.

Awali idadi ya majeruhi 46 walisafirishwa kutoka Morogoro mpaka Muhimbili kwa matibabu ya kibobezi.

Mpaka kufikia leo, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa Muhimbili, Amini Algaesha idadi ya majeruhi waliosalia hospitalini hapo ni 32, kati yao 17 wapo kwenye chumba cha wagonjwa mahututi

Wengi wa majeruhi waliokimbizwa Muhimbili walikuwa wameunguzwa na moto kwa asilimia 80 na kuendelea.

Mkasa huo ulitokea majira ya saa mbili asubuhi ya Jumamosi baada ya lori lililobeba shehena ya petroli kuanguka katika mji wa Morogoro, na watu kuanza kuchota mafuta yaliyomwagika kisha mlipuko mkubwa kutokea.

Kumekuwa na hisia tofauti juu ya ajali hiyo lakini Rais John Magufuli amewataka wananchi kuacha kuhukumu waliofariki na majeruhi.

''Naona watu wanasema kwamba hawa wote walienda kuiba , tusiwe majaji wengine walienda kusaidia huku wengine wakiwa wapita njia , Mwengine alikuwa safarini kuelekea Mtwara, akazuiliwa na moto ulipolipuka ukamkuta'', alisema Magufuli baada ya kuwajulia hali majeruhi siku ya Jumapili.

Baadhi ya waliofariki waliungua kiasi cha kutokutambulika na vipimo vya vinasaba vya jeni (DNA) kupitia ndugu waliopoteza wapendwa wao.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.