IGP Sirro: Tupo makini tishio la ugaidi

IGP Sirro: Tupo makini tishio la ugaidi

20 June 2019 Thursday 06:21
IGP Sirro: Tupo makini tishio la ugaidi

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
JESHI la polisi limewatoa hofu wananchi juu ya tishio la ugaidi katika maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam, likisema lilikuwa na taarifa hizo na kwamba zimeshaanza kufanyiwa kazi.

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) nchini Tanzania, Simon Sirro amesema jeshi lilipata fununu za shambulio hilo kabla Ubalozi wa Marekani kutoa tahadhari juu ya tukio hilo kupitia tovuti yake Juni 18,2019.
Kuhusu tahadhari iliyotolewa na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania Sirro alisema: "hiyo ni taarifa kama taarifa nyingine, inaweza kuwa ya kweli au uongo, lakini sisi kama vyombo vya ulinzi huwa hatupuuzi jambo''.

Aliongezea kuwa walipata taarifa kuhusiana na tishio hilo tangu siku ya Jumanne Juni 17, 2019  na kwamba timu  za operesheni na intelijensia na wengine wanaifanyia kazi.

Katika tangazo lake Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa tahadhari kuwa kuna fununu za mipango ya mashambulizi jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa tahadhari hiyo iliyochapishwa kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Ubalozi huo, eneo la Masaki ndilo linalolengwa.

Eneo hilo lililopo kwenye rasi ya Msasani ni moja ya maeneo ya makazi ya kigahari zaidi jijini humo.

Tahadhari hiyo inabainisha kuwa, maeneo yanayolengwa ni mahoteli na migahawa ambayo hutembelewa na watalii ikiwemo eneo maarufu la maduka ya Slipway.

"Ubalozi hauna ushahidi wa moja kwa moja wa tishio hilo ama taarifa za muda gani mashambulizi yatatokea, hata hivyo unawaonya wananchi kuchukua tahadhari."

Ubalozi huo aidha umewataka wakazi, kujiepusha na makundi na kufuatilia taarifa kupitia vyombo vya habari.

Updated: 20.06.2019 08:06
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.