January Makamba atoa neno la mwisho kwa Magufuli

January Makamba atoa neno la mwisho kwa Magufuli

22 July 2019 Monday 15:24
January Makamba atoa neno la mwisho kwa Magufuli

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
SAA takriban 30 baada ya aliyekuwa waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa rais(Muungano na Mazingira) January Makamba kuondolewa madarakani, ametoa la moyoni.


Hii leo Julai 22, 2019 kupitia ukurasa wake wa Twitta amesema; Neno la mwisho kwenye hili: ''Namshukuru Rais kwa kuniamini, Makamu wa Rais kwa kunielekeza, PM kwa kunisimamia, na Team ya VPO/NEMC na Mawaziri wote kwa ushirikiano. Nampongeza @HusseinBashe na Simbachawene kwa kuaminiwa. Nawatakia heri na kuwaahidi ushirikiano wangu wa dhati'' 


Julai 21, 2019 rais Magufuli alitangaza kumfuta kazi January  na nafasi yake kuchukuliwa na George  Simbachawene ambaye ameapishwa  leo jijini Dar es Salaam.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.