JKT yapata bosi mpya

JKT yapata bosi mpya

11 September 2019 Wednesday 15:36
JKT yapata bosi mpya

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

RAIS John Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

Mbuge anachukua nafasi Meja Jenerali Martin Busungu ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Akiba.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo.

Awali Aprili13, Rais Magufuli alimpandisha cheo Brigedia Jenerali Mbuge kutoka kuwa Luteni Kanali na kuwa Brigedia Jenerali.

Dk. Magufuli alimpandisha cheo hicho Brigedia Jenerali Mbuge baada ya kufurahishwa na utendaji wake wa kazi katika kusimamia ujenzi wa miradi mbalimbali ya Serikali ikiwamo ujenzi wa ukuta wa Mirerani.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.